Alhamdulillah nilifika London Jana na nipo hapa kwa mualiko kutoka Chuo kikuu cha Soas,Idara ya Masomo ya kiafrika.
Nitawasilisha mada kuhusu "MCHANGO WA FASIHI KATIKA HIP HOP" kwenye Kongamano la Baraza la Kiswahili kesho In Shaa Allah.
Taarifa zaidi zitawajia.
Ijumaa yenye Baraka sana kukutana na Professor Assad katika sala ya Jumaa pale Masjid Imam Jabir Bin Zaid , alikuwa anamaliza kusali sunnah nikamsubiri nikajitambulisha akauliza, unapiga Hip Hop ya ipi? Yenye Ujumbe mwingi au ya siku hizi? nikamwambia Napiga Yenye Ujumbe mwingi
Taifa Stars bila hamasa
Taifa Stars isiyo ya Wachambuzi
Taifa Stars iliyotelekezwa
Taifa Stars ya Hip Hop
Taifa Stars isiyoenda na Vikosi vya Wajuaji
Taifa Stars isiyo haidiwa hela
Taifa Stars iliyopangwa na kuchaguliwa na kocha.
Huwa inaenda vizuri kabisa.
TAARIFA.
Jana katika Darasa la Hip Hop na Diplomasia katika Chuo Kikuu cha North Carolina U.S.A chini Professor Mark Katz, ambaye ni mkuu wa Idara ya Muziki chuoni hapo,walitumia wimbo Wangu wa "NIANZIE WAPI" Kujifunza na kuibua mjadala juu ya Siasa na Jamii.