Msamaha Na Upatanisho
Msamaha Na Upatanisho
MSAMAHA NA UPATANISHO
na
Jonathan M. Menn
Mei 2007; toleo jipya Mei 2013; imesahihishwa Julai 2014; imesahihishwa Novemba 2017
YALIYOMO
MSAMAHA…...………………………………………………………………………………………………….2
UPATANISHO………………………………………………………………………………………...…..........26
NUKUU ZILIZOTUMIKA……….…………………………………………………………………………...33
NYONGEZA: Mfano wa Msamaha wenye msingi wa maamuzi kwa ajili ya urejesho wa Ndoa na
Mahusiano ya Kifamilia…..…………..................................................................................................34
MWANDISHI…..…………………………………………………………..…………………………………..37
1
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
MSAMAHA
1
Nukuu zote za Biblia zimetoka katika toleo la New American Standard ikiwa vinginevyo imeelezwa.
2
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
II. Sisi Tumeagizwa na Kristo—kama kiini cha maana ya kuwa Mkristo—kusamehe wengine
A. Sala ya Bwana inatutaka sisi kusamehe wengine kama sisi tulivyosamehewa: 9 Basi ninyi salini hivi; Baba
yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe.10 Ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko
mbinguni. 11Utupe leo riziki yetu. 12Utusamehe deni zetu,kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. 13Na
usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata
milele. Amina. 14Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
15
Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. (Math 6:9-15)
Kifungu kinachofanana na hicho ni Luka 11:2-4.
1. Zinagatia kwamba sehemu ya sala ya Bwana ambayo Yesu alisisitiza kipekee na kupendekeza ni
sehemu ya maombi inayohusu kusamehe.
2. Zingatia kwamba kutokusamehe pia ni dhambi.
3. Zingatia hatimaye kuwa Yesu ameweka wazi kabisa kwamba msamaha wa Mungu kwetu
unategemeana sana na msamaha wetu kwa wengine: Mungu atatusamehe sisi ikiwa sisi tutawasamehe
wengine; lakini Mungu hatatusamehe sisi kama hatutawasamehe wengine. Kama D. A. Carson
anavyoeleza kuwa: “Watu hujikosesha haki wenyewe ya kusamehewa kama wakiwa wagumu katika
kung’ang’ania uchungu kiasi kwamba hawawezi au hawapo tayari kusamehe wengine. Katika hali hizo,
hawaonyeshi kuvunjika, toba, hawatambui thamani kuu ya msamaha, hawana uelewa wa hali zao mbaya
za dhambi, hawana toba” (Carson 2002: 79)2
B. Mfano mrefu sana wa Mathayo3 ni juu ya umuhimu wa kusamehe wengine: 21 Kisha Petro akamwendea
akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba? 22 Yesu
akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini. 23 Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni
umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake. 24 Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu
mmoja awiwaye talanta 25 Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe,yeyena mkewe na watoto
wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni. 26 Basi yulemtumwa akaanguka, akamsujudia akisema,
Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia. 27 Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua,
akamsamehe ile deni. 28 Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari 29 Basi
mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia. 30 Lakini
hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni. 31 Basi wajoli wake walipoyaona
yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka. 32Ndipo bwana wake
akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; 33 nawe, je!
Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe? 34 Bwana wake akaghadhibika,
akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote. 35 Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni
atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.” (Math 18:21-35)
C. Yesu mfano wake mrefu kuliko yote ni katika Luka (na katika Biblia)ni juu ya msamaha na urejesho: 11
Akasema, Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; 12 yule mdogo akamwambia babaye, Baba, nipe sehemu ya mali
inayoniangukia. Akawagawia vitu vyake. 13 Hata baada ya siku si nyingi,yulemdogo akakusanya vyote, akasafiri
kwenda nchi ya mbali; akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati.
14
Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji. 15 Akaenda
akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe.
16
Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu.
17
Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza,
na mimi hapa ninakufa kwa njaa. 18 Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa
juu ya mbingu na mbele yako; 19 sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.
20
Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma,
akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana. 21 Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya
mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena. 22 Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni
upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni; 23 mleteni ndama yule aliyenona
2
Randy Alcorn analiweka hivi: “Hatumwumizi yeyote kupitia uchungu kwa kiwango ambacho tunajiumiza wenyewe. Mtu
Fulani aliniambia, ‘Uchungu ni sawa na kunywa sumu na kungoja mtu mwingine afe.’” (Alcorn 2009: 425)
3
Mfano wa Yesu kuhusu watumwa wawili (Math 18:21-35) una maneno 245 katika kifungu cha kiyunani, ikihusisha swali
la Petro la kwamba mara ngapi tuwasamehe wengine wanaotukosea, Nini tukio la mfano, na maneno yanayotambulisha
mfano wa Yesu, “Yesu akamwambia.” Mfano wa pili wa Yesu kwa urefu, wafanyakazi katika shamba la mzabibu (Math
20:1-16), una maneno 241 maneno ya kiyunani (yakihusishwa maneno mawili ambayo asili yake inatiliwa mashaka sana);
ingawa maneno hayo yote, ni maneno ya Yesu mwenyewe. (Aland, et al.: 2001)
3
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
mkamchinje; nasi tule na kufurahi; 24 kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa
amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia. 25 Basi, yule mwanawe mkubwa alikuwako shamba na
alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na machezo. 26 Akaita mtumishi mmoja,
akamwuliza, Mambo haya, maana yake nini? 27 Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba yako amemchinja
ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yu mzima. 28 Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye
alitoka nje, akamsihi. 29 Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala
sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwanambuzi, nifanye furaha na rafiki zangu; 30 lakini,
alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona.
31
Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako. 32 Tena, kufanya
furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea,
naye ameonekana’” (Luka 15:11-32)
D. Yesu anaunganisha msamaha wetu na upendo wetu: 36 Mtu mmoja katika Mafarisayo alimwalika ale
chakula kwake; akaingia katika nyumba yake yule Farisayo, akaketi chakulani. 37 Na tazama, mwanamke
mmoja wa mji ule, aliyekuwa mwenye dhambi, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya
yule Farisayo, alileta chupa ya marimari yenye marhamu. 38 Akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia,
akaanza kumdondoshea miguu machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake, akiibusubusu miguu
yake na kuipaka yale marhamu. 39 Basi, yule Farisayo aliyemwalika alipoona vile, alisema moyoni mwake, Mtu
huyu kama angekuwa nabii, angemtambua mwanamke huyu amgusaye, ni nani, naye ni wa namna gani, ya
kwamba ni mwenye dhambi. 40 Yesu akajibu akamwambia, Simoni, nina neno nitakalo kukuambia. Akasema,
Mwalimu, nena. 41 Akasema, Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili; mmoja amwia dinari mia tano,
na wa pili hamsini. 42 Nao walipokuwa hawana cha kumlipa, aliwasamehe wote wawili.Katika hao wawilini
yupiatakayempenda zaidi? 43 Simoni akajibu akasema, Nadhani ni yule ambaye alimsamehe nyingi.
Akamwambia, Umeamua haki. 44 Akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, Wamwona mwanamke
huyu? Niliingia nyumbani kwako, hukunipa maji kwa miguu yangu; bali huyu amenidondoshea machozi miguu
yangu, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake. 45 Wewe hukunibusu; lakini huyu tangu nilipoingia
hakuacha kunibusu sana miguu yangu. 46 Hukunipaka kichwa changu mafuta; bali huyu amenipaka miguu
yangu marhamu. Luka 7 47 Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa
kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo. 48 Kisha alimwambia mwanamke,
Umesamehewa dhambi zako. 49 Ndipo wale walioketi chakulani pamoja naye walianza kusema mioyoni mwao,
Ni nani huyu hata asamehe dhambi? 50 Akamwambia yule mwanamke, Imani yako imekuokoa, enenda zako kwa
amani. (Luka 7:36-50)
E. Yesu anaunganisha kipekee kusamehe kwetu wengine na maisha yetu ya maombi na msamaha wa Mungu
kwetu: 23 “Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka
moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. 24 Kwa sababu hiyo nawaambia,
Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. 25 Nanyi, kila msimamapo
na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa
yenu. 26 Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.”
(Marko 11:23-26)
1. Zingatia kuwa Yesu alitoa tamko hili wakati alipoingia Yerusalemu kwa shangwe, muda mfupi kabla
ya kusulubiwa kwake. Ingawa yote aliyoyasema Yesu ni muhimu, maneno yaliyosemwa wakati kifo
kinamfikia mtu yana umuhimu unaozidi.
2. Zingatia pia kwamba Yesu aliyarudia maneno aliyoyasema aliposisitiza na kushauri juu ya umuhimu
wa msamaha katika sala ya Bwana. Matamko yanarudiwa kwa kusudi la kutilia mkazo umuhimu wake.
III. Mitume hutueleza sisi kuwasamehe wengine, kama sheria na kuonyesha kielelezo
A. Paulo anatuagiza kusamehe: Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na
Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi. (Waef 4:32; tazama pia 2 Wakor 2:7; Wakol 3:13)
Maoni ya Carson kuhusu mstari huu: “Wazo si kwamba sisi tumesamehewa, na kwa hiyo tunatakiwa
kusamehe, lakini kwamba Mungu mwenyewe, katika Kristo, ametusamehe, na kwa hiyo deni letu halipimiki.
Haijalishi ni ubaya mkubwa kiasi gani tuliofanyiwa, ni kidogo ukilinganisha na uovu tuliofanya mbele za uso
wa Mungu. Pamoja na hayo Mungu katika Kristo akatusamehe sisi. Ikiwa tunajua chochote kitupasacho kutoa
msamaha, ikiwa tumevumbia chochote kuhusu ukubwa wa deni tunalowiwa na Mungu, sisi kuwasamehe
wengine hakutakuwa jambo gumu.” (Carson 2002: 80-81)
4
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
B. Aina ya msamaha wa Paulo: 10 Lakini kama mkimsamehe mtu neno lo lote, nami nimemsamehe; kwa maana
mimi nami, ikiwa nimemsamehe mtu neno lo lote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele za Kristo, 11 Shetani asije
akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake. (2 Wakor 2:10-11)
1. Zingatia kuwa Paulo kuwasamehe wengine ni kwa ajili ya kanisa (“kwa ajili yenu”). Zaidi, mara zote
alijua anachofanya (i.e., ikiwa anasamehe au hasamehi) hayo yanafanyika “katika uwepo wa Kristo.”
2. Zingatia pia kwamba kutosamehe kutamfanya shetani “atushinde sisi.”
3. Kilicho kweli kwa Paulo ni kweli kabisa kwetu, hasa sisi ambao (kama Paulo) tupo kwenye nafasi ya
uongozi wa kanisa:
a. Ikiwa tunasamehe au hatusamehi kanisa linaathirika kwa wema au kwa ubaya .
b. Ingawa hatumwoni yeye wala hatumhisi, kila tufanyacho (ikiwa ni pamoja na kusamehe au
kutokusamehe ubaya uliotendwa dhidi yetu na wengine) kinafanyika katika uwepo wa Kristo—
na tutahukumiwa na Kristo ikiwa hatusamehi.
c. Kutokusamehe kwetu kunampa shetani fursa na faida ya kufanya kazi kupitia sisi, na kinyume
chetu, ndani na kinyume cha kanisa. Kutosamehe kwetu kutasababisha wengine kufuata mfano
wetu mbaya na kutosameheana—kanisa kwa njia hiyo litakuwa na mgawanyiko, litagawanyika,
na lenye uchungu; na katika hali hiyo shetani peke yake tu ndiye anayefanikiwa. Kwa upande
mwingine, kama tutakuwa na roho ya msamaha, washirika kanisani watafuata mfano wetu.
Ikiwa tunasamehe tutaweza kuhubiri vifungu vyote vya Biblia kwa nguvu za Roho Mtakatifu,
bila ya kuwa wanafiki. Katika hali hii, shetani hatapata fursa na faida ya kufanya kazi kupitia
sisi au kupitia kanisa.
C. Stephano, shahidi wa kwanza wa kanisa, ametupa mfano mkuu (baada ya Yesu mwenyewe), kwa
kuwasamehe wale waliomwua, hata wakati anakata roho: 59 Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba,
akisema, “Bwana Yesu, pokea roho yangu.” 60 Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, “Bwana, usiwahesabie
dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala.” Na Sauli alikuwa akiona vema kwa kuuawa kwake. (Matendo 7:59-
60)
I. Nini SI msamaha4
A. Msamaha SI “kuita ubaya wema,” kupunguza maumivu, kuvumilia ubaya, kusema “ulichofanya si
kikubwa sana,” au “si kitu,” au kuwa na “kutokujali” kuhusu ubaya au kwa aliyefanya ubaya
1. Msamaha ni kutambua kwamba alichotufanyia mtu mwingine NI ubaya. Hakika, kile alichofanya mtu
mwingine ni kibaya sana hata Yesu akawa radhi kuteswa na kuawa kwa dhambi hiyo hiyo (vile vile
kama kwa dhambi zetu zilivyo mbaya).
2. Kusema kuwa ubaya ni wema, au “si jambo la kutilia maanani,” au “hakuna shida” ni kuacha kweli—
kwa hiyo inatutenga sisi kutoka kwa Mungu na Kristo, kwa sababu Mungu ni kweli (Kutoka 34:6;
Zaburi 25:5, 10; 33:4; 40:10-11; 43:3; 57:10; 86:15; 89:14; 117:2; 119:142, 151; 138:2; Isaya
65:16); Kristo ni kweli (Math 22:16; Marko 12:14; Yoh 1:14, 17; 3:21; 8:45-46; 14:6; 18:37; Waef
4:21); na sisi tunategemewa kuwa wakweli kwetu sisi wenyewe, mbele za Mungu na kwa wengine
(Zaburi 51:6; 86:11; 145:18; Mithali 3:3; 16:6; 23:23; Yoh 4:23-24; Waef 4:25).
3. Msamaha si kuvumila. Tunapomsamehe mtu haimaanishi tunavumilia kile alichofanya, au
tunamkaribisha atuumize tena, au tunataka itokee tena. Msamaha unahitaji jicho la wazi kujua tofauti
kati ya wema na ubaya, na kuayaita mambo vile yalivyo,-kwa sababu unaweza tu kusamehe “ubaya”
mkubwa unaoweza kukuumiza.
4
Hii sehemu kwa ujumla imezingatia kwa Jeffress 2000: sura za. 3 na 7; Smedes 1984: sura ya. 5; Smedes 1996: sura. 2-3;
Enright 2001: sura. 2; na Klassen n.d.: “Definitions.”
5
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
kwa kumwua yeye. Tunapokuwa watii kwa Mungu, katika kweli ya Neno lake, na katika nguvu ya
Roho wake, atatupa sisi imani na uwezo wa kufanya jambo gumu, kwa sababu ni jambo sahihi-
kusamehe wale waliotujeruhi na kutuumiza sana. (Warumi 4:19-22; 14:4; 1 Wakor 10:13; Waef 3:20-
21; 6:10-16; Waeb 2:18; 7:25; Yuda 24).
3. Mtu anaweza kudhani msamaha unatoa wajibu mkubwa sana kwa aliyekosewa kuliko aliyekosa.
Ingawa, Jeffress anaeleza: “Mungu hatuondolei majukumu kwa sababu hayatufurahishi au magumu.
Kwa mfano, zingatia haya maneno maarufu ya Yesu ya hotuba yake ya mlimani:
Mmesikia kwamba imenenwa, ‘Jicho kwa jicho, na jino kwa jino.’ Lakini mimi nawaambia,
Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la kushoto na
mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. Na mtu
atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili. [Math 5:38-41]
Zingatia kwamba kila hali ambayo Yesu anaitaja hapa, haweki majukumu kwa mkosaji, lakini kwa
aliyekosewa. Aliyekosewa anatakiwa kugeuza shavu lingine, atoe kanzu yake vile vile kama joho lake,
na kwenda maili ya pili.” (Jeffress 2000: 45; tazama pia Sande 2004: 148-49; na Worthington 2003: 68,
“Hatusamehi kwa sababu ni rahisi, lakini kwa sababu ni haki na ni mwitikio kwa upendo wa Mungu na
msamaha wake kwetu.”)
4. Ikiwa unadhani kumsamehe mtu fulani aliyekukosea kunakuondolea “hadhi” au “utu,” zingatia hili:
Hilo ndilo unalowaza kuhusu Kristo? Je yeye kwa kiasi ameshuka “hadhi” kwa sababu amekusamehe
wewe?
C. Kusamehe SI kusahau
1. “Kusaha ni mchakato usiotumia nguvu wala akili unofanya jambo kutoweka kwenye kumbukumbu
kutokana na muda kupita. Kusamehe ni mchakato mtambuka; unahusisha uchaguzi wa kudhamiria na
tendo hasa la kujitoa.” (Sande 2004: 206).
2. Huwezi kusamehe kile ambacho umesahau. Ingawaje, punde tu tunaposamehe tunaweza kusahau kwa
sababu tumeponywa.
3. Baadhi ya vifungu husema Mungu “husahau” dhambi zetu (tazama Zab 103:12; Yeremia 31:34;
Mika 7:19).
a. Mistari ile, kama rejea za Biblia kuhusu “macho” ya Mungu (2 Nyakati 16:9), “masikio”
yake (1 Pet 3:12), “mikono” yake (Kutoka 24:11), na “miguu” yake (2 Samweli 22:10) ni
“kumpa Mungu sifa za kibinadamu,” bila shaka nayo ni, kujaribu kumwelezea Mungu asiye na
mwisho kwa kutumia mifano ya mwanadamu aliye na mwisho. Haileti maana kuamini kwamba
Mungu anayejua yote ghafla anapoteza kumbukumbu na kusahau kabisa kile kilichofanywa na
viumbe vyake.
b. Kwa hakika, Biblia huweka wazi kwamba matendo yetu yote, na nia zetu, yote mabaya na
mema, yatahukumiwa na Mungu na kuamua kuhusu thawabu yetu ya milele (Math 16:27;
Luka 8:17; 12:2-3; Warumi 2:1-16; 14:10-12; 1 Wakor 3:12-15; 2 Wakor 5:10; Ufunuo
20:11-15; 22:12). Hii inaonyesha kwamba Mungu ni lazima aweke kumbukumbu ya matendo
yetu ili atuhukumu kwa haki.
4. “Mistari ya Biblia inayoongelea Mungu kusahau dhambi inajaribu kuelezea msamaha wa Mungu wa
kisheria kwa dhambi zetu. Tunapopokea msamaha wa Mungu hatupaswi tena kuogopa adhabu ya milele
kwa ajili ya dhambi zetu.” (Jeffress 2000: 129). Ukweli huu umeelezwa kwa wazi katika Warumi 4:7-8
(ambayo inanukuu Zab 32:1-2): 7 Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake. 8Heri
Bwana asiyemhesabia upotovu, Ambaye rohoni mwake hamna hila.
Jeffress anaelezea: “Dhambi zetu zinatufanya wadeni kwa Mungu. Tunawiwa na Mungu kwa
dhambi tulizomtendea. Lakini kifo cha Kristo kimelipa deni katika ule muamala ambao Paulo anaueleza
kwenye Wakolosai 2:13-14: … akiisha kutusamehe makosa yote; akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa
ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea
msalabani. Tunapokuwa Wakristo, anachukua deni analokudai, analigongomea msalabani, na kutangaza
limelipwa lote.’ Lakini ni rahisi kusamehe deni bila ya kulisahau.” (Jeffress 2000: 130)
5. Kwa namna nyingine kusema Mungu “husahau” makosa yetu ni kusema kwamba yeye hisia yake
kwetu ni kana kwamba hakumbuki. Au, “wakati Mungu anaposema kwamba hakumbuki tena dhambi
zako’ (Isaya 43:25), hasemi kwamba hawezi kukumbuka dhambi zetu. Bali, anaahidi kwamba
hatazikumbuka. Anapotusamehe, anaazimia kutozitaja, kutozihesabu, au kutofikiri tena kuhusu dhambi
zetu kamwe.” (Sande 2004: 206)
6
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
D. Kusamehe SI kujitetea
1. Kujitetea ni kinyume cha kusamehe. Tuna tetea watu tunapotambua kwamba hawapaswi kulaumiwa
kwa jambo walilofanya, au kwa matokeo mabaya yaliyotokea kwa bahati mbaya kutokana na matendo
waliyotenda kwa nia njema; Tunawasamehe watu tunapotambua kuwa wanapaswa kulaumiwa kwa
jambo walilofanya—jambo ambalo ni kosa na halina utetezi—yakiwemo yale matendo mabaya ambayo
kwa hayo walilenga kutuumiza sisi.
2. “Msamaha unasema, ‘wote wawili tunajua ulichofanya ni kibaya na ni bila kujitetea. Lakini kwa
kuwa Mungu amenisamehe mimi, nami nakusamehe wewe.’ Kwa sababu msamaha hushughulikia
dhambi kiuhalisia, unaleta uhuru ambao hakuna kiwango cha kujitetea kinaweza kuutoa.” (Sande 2004:
206-07)
F. Msamaha hautoi nafasi ya “kupuuzia haki” na HAUTOI “uhuru” kwa watu kuendelea na dhambi zao,
lakini si lazima uondoe matokeo yote ya ubaya
1. Msamaha ni kwa ajili ya mahusiano binafsi na ni kwa ajili ya kuponya majeraha ya ndani yako
mwenyewe ambayo yametokana na ubaya uliofanyiwa-msamaha ukitumiwa kivitendo, ni jambo
tunalofanya ndani ya mioyo yetu, ufahamu na nafsi. Unafanyika kwa kumtii Kristo, na kimsingi unaleta
uponyaji wetu wenyewe. Haki katika jamii ni wajibu wa raia na mfumo wa makosa ya kijinai na ni kwa
kusudi la kurekebisha uovu unaotendwa dhidi ya jamii. Sisi kuwasamehe wengine haimaanishi wao
hawana “hatia” na inaweza isikubalike kisheria; haiondoi au haipo juu ya adhabu za kimahakama za
mfumo wa nchi wa haki za raia na makosa ya kijinai, kwa sababu ubaya uliotendwa dhidi yetu unaweza
kuwa ni ubaya unaoathiri nchi, na jamii au binadamu kwa ujumla.
2. Unasamehe uovu uliotendewa wewe; huwezi kusamehe mtu kwa ubaya aliofanya kwa mtu mwingine,
au uliofanywa dhidi ya nchi au wanadamu kwa ujumla-huko ni kuachilia. Mtu akimwumiza mtoto
wangu, hilo linaweza likaniumiza mimi pia, kwa sababu nampenda mtoto wangu. Ninaweza
kumsamehe aliyetenda kosa nisiwe na hasira dhidi yake, nisiwe na uchungu na maumivu mengine
ambayo yamenipata kutokana na alichofanya kwa mtoto wangu, lakini siwezi kumsamhe mkosaji kwa
niaba ya mtoto wangu kwa kosa lililofanyika kwa mtoto. Mtoto wangu mwenyewe atapaswa kupitia
mchakato wa kumsamehe mkosaji kwa kosa alilofanya kwake.
3. Uelewa kuhusu matokeo ya dhambi unatakiwa utusaidie kuelewa kwa nini sisi ni wenye dhambi
wabaya zaidi kuliko tunavyojiona-dhambi moja huathiri watu wengi zaidi ya vile tunavyoweza kuwaza.
Hiyo ndiyo sababu tunamhitaji Kristo atusamehe sisi—kwa sababu alizichukua dhambi zetu zote juu ya
nafsi yake mwenyewe. Tunapotambua kina cha dhambi zetu, na kiwango cha msamaha wa Kristo
kwetu, tunapaswa kuwa wepesi kuweza kusamehe wengine kwa makosa waliyotutendea.
4. Mwisho, Haki itapatikana kwa Mungu katika hukumu yake ya mwisho; huo si wajibu wetu. Sisi
tukimsamehe mkosaji hiyo haimwondolei hatia yake mbele za Mungu na haibadilishi haki ambayo
Mungu atatoa katika hukumu ya mwisho.
5. Msamaha haupunguzi ubaya wa matendo mabaya.
a. “Hakuna msamaha halisi bila ya kuwepo kwanza kwa uwazi na ukweli wa hukumu” (Smedes
1984: 79). Kila mtu anahisi maumizi yeye binafsi; kiwango cha maumivu yake hakiongezeki
kwa sababu mtu ameumiza jozi, au mamia, au maelfu au hata mamilioni ya wengine—kila
mwathirika anahisi kwa kipimo kilichojaa cha maumivu yake hata kama mamilioni wengine
wameumizwa.
b. Kusema kwamba baadhi ya “majitu” hawasameheki inashangaza inawafanya wawe vile
wanavyotaka inawainua na kuwafanya—inawainua kuwa “binadamu wa ajabu” wenye hadhi,
kama ya shetani. Cha kushangaza, hilo linawatoa katika kuhitaji msamaha, au kutoka kwenye
wajibu wa kibinadamu, kwa sababu wao ni zaidi ya binadamu. Hii inasababisha mtazamo
uliopotoka kwamba waathirika ni lazima waishi na siku zote na majeraha yao na maumivu, kwa
sababu kamwe hawataponywa majeraha kupitia msamaha. Kwa kuwaona “majitu” (wauaji wa
halaiki, waasi wa kisiasa katika historia, nk.) kana kwamba kwa kiasi fulani ni “tofauti” na sisi
7
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
wengine wote, “wakubwa” kuliko sisi, inatufanya tuwe wadogo na ni kinyume na kweli. Ukweli
ni kwamba “watu wa kawaida sana hufanya ubaya usio wa kawaida” (Smedes 1984: 81).
c. Mwandishi wa Kirusi Aleksandr Solzhenitsyn alivumbua: “Kama tu ingelikuwa rahisi! Kama
kungekuwa na watu wabaya mahali fulani kwa siri wakitenda mabaya, ingekuwa lazima
kuwatenga na sisi tuliobaki na kuwaangamiza. Lakini mstari unaotenga kati ya ubaya na wema
hupita katikati ya moyo wa kila mwanadamu. Na ni nani aliye tayari kuangamiza kipande cha
moyo wake mwenyewe?” (Solzhenitsyn 1985: 75)
6. Unapomsamhe aliyekukosea na kukuumiza, unachofanya si lazima kiondoe matokeo ya makosa kwa
mkosaji.
a. “Matokeo ya kiasili ya matendo yamepangwa vizuri na Mungu na yanatufanya tuwe watu
ambao tunatakiwa kuwa. Kuyapunguza makali inaweza kuwa ni kuwaumiza wale ambao
walikusudiwa kusaidika.” (Willard 1997: 262) Kwa mfano, Daudi alipofanya uzinzi na
Bathsheba na kusababisha mume wake Uria Mhiti kuawa, ingawa Mungu alimsamehe Daudi
dhambi yake, hata hivyo Mungu alieleza kwamba: “upanga hautaondoka nyumbani mwako . . .
Nitakuondokeshea uovu katika nyumba yako, nami nitawatwaa wake zako mbele ya macho
yako, na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako mbele ya jua hili. Maana wewe ulifanya
jambo lile kwa siri; bali mimi nitalifanya jambo hili mbele ya Israeli wote na mbele ya jua. [na]
kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za Bwana nafasi kubwa ya kukufuru, mtoto
atakayezaliwa kwako hakika yake atakufa.” (2 Samweli 12 7-14)
b. “Mkosaji hayupo ‘nje ya ndoano’ tunaposamehe; tunagundua kwamba ‘sisi tunakuwa nje ya
ndoano’ tunaposamehe” (Klassen n.d.: n.p.). Anaongeza, “Ninaposamehe ninamweka mfungwa
huru na hapo ninagundua kwamba mfungwa ni mimi” (Ibid.).
7. Vivyo hivyo unapomsamehe mtu aliyekukosea na kukuumiza, siyo lazima matokeo ya lile kosa
ulilotendewa yaondoke kwako. Kwa mfano, “Ninaweza kumsamehe mtu aliyenipofusha, lakini
kusamehe kwangu hakutanirudishia kuona” (Klassen n.d.: n.p.). Hata hivyo, ni muhimu kutambua
kwamba, ingawa “kusamehe hakuondoi maumivu . . . msamaha hutusaidia sisi kuchukuliana na
maumivu” (Ibid., anasisitiza na anaongezea). Zaidi, Mungu hutumia msamaha (ambao ni utii wetu
kwake) kutubadilisha sisi na kutufanya tuzidi kufanana na Kristo, kutuvuta karibu na yeye, na kutupa
ufunuo, huruma na unyenyekevu. Katika mchakato (na unaweza kuwa mchakato mrefu—kwa hakika,
mchakato wa maisha yote), tunapofikia kujua makusudi yake katika majeraha na kutenda kwake kazi
katika maisha yetu kwa njia ya majeraha na kwa njia ya msamaha wetu, atabadilisha maumivu na
kuyaondoa mbali.
G. Msamaha HAINA maana uendelee kumtumaini mkosaji, au kuendelea na urafiki, au katika mahusiano
na yeye.
1. Msamaha unatolewa; kuaminika kunatafutwa. Urafiki unahitaji kuaminiana na kuheshimiana kwa
pande zote. Heshima, kama kuaminika, inatafutwa.
2. Anahitajika mtu moja ili kusamehe; Wanahitajika watu wawili ili kupatana. Msamaha ni jambo
linalotokea ndani ya mtu anayefanya hivyo” (Smedes 1996: 25). Smedes anaongeza, “Tunasamehe
ndani ya mioyo yetu na ufahamu wetu; yanayotokea kwa wale tunaowasamehe yanawategemea wao”
(Ibid.: 177). Siyo jambo linalofanana na upatanisho, inagwa ni sehemu ya upatanisho—msamaha
unatangulia upatanisho:
a. Msamaha ni mwitikio wa kimaadili kwa mwingine aliyetenda kinyume na maadili.
b. Upatanisho ni kuja pamoja kwa watu wawili kurejesha mahusiano yaliyopoteza kuaminiana
(kuondoa kizuizi cha mahusiano mazuri).
3. Ni kweli tunapaswa “kuwapenda adui zetu, kuwaombea wale wanaokuudhi” (Math 5:44);
“wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale wanaowachukia ninyi” (Luka 6:27); na “wapendeni
adui zenu, watendeeni mema” (Luka 6:35). Yesu alisema kwamba amri ni, “mpende jirani yako kama
unavyojipenda mwenyewe,” pamoja na kumpenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, nafsi, na
akili ni msingi kwa “sheria yote na manabii” (Math 22:37-40).5
a. Zinagatia kwamba Yesu hakusema tunatakiwa “kuwakubali” adui zetu. Alitambua kwamba
kwa hakika kwamba, tutakuwa na maadui watakaotutesa. Hata hivyo tunatakiwa “kuwapenda”
5
Rejea yake “Sheria yote na Manabii” anarejea Biblia nzima (Agano la Kale)—nayo ni., Neno lote la Mungu lililofunuliwa
kwa ajili ya jinsi tunavyotakiwa kuishi. Paulo vilevile alisema, “Biblia nzima inatimizwa katika neno moja, katika tamko
kwamba, ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako”’ (Wagal 5:14). Tamko kwamba “mpende jirani yako kama nafsi yako”
linatoka katika Mambo ya Walawi 19:18.
8
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
wao. Na tena aliongeza kwamba, “kama wewe utawapenda [tu] wale wanaokupenda, utapata
thawabu gani? Je hata watoza ushuru hawatendi vivyo hivyo?” (Math 5:46)
b. Maana na kusudi la upendo huo ni hii: “Mtu kuwapenda jirani, adui zake . . . si lazima iwe ni
kutenda kile kinachowapendeza, lakini ni kuchagua kuwaonyeshea upendeleo na nia njema . . .
Mtu anatakiwa atambue uhitaji wa watu kubadilishwa kwa njia ya neema ya Kristo, na kufanya
kila liwezekanalo ili kuwaleta katika maarifa ya Bwana. Hili linaweza kuhusisha matendo ya
ukarimu au hata marudi na kunidhamisha, yote ikiwa ni kazi ya upendo. . . . Tukirejea upendo
wa Mungu [ambao tunatakiwa kuuonyesha], ni mapenzi makamilifu ya Mungu kwa
mwanadamu. Inahusisha utendaji wa Mungu wa yale anayojua kwamba ni mema kwa ajili ya
mtu na siyo lazima yawe ni yale anayotamani mtu.” (Zodhiates 1993: agapáō; agápē)
c. Kwa hiyo, kupenda si kumchukia mkosaji, hata kama amekuumiza, bali kufanya kwa ajili ya
usalama wake, kumwonyesha ukarimu na wema, kujitoa kibinafsi kama sadaka. Kupenda
kunahusisha kusamehe. Kupitia hili, Mungu anaweza kubalisha hisia dhidi ya mkosaji kwa
kadiri anavyokubadilisha na kuondoa maumivu unayohisi kama matokeo ya kosa.
d. Kumpenda adui au jirani yako haimaanishi umwache aendelee na njia yake, au umtumaini
baada ya kumthibitisha kuwa hastahili, au uendelee naye katika biashara baada ya
kumthibitisha kuwa ni mtu asiyejua biashara, au uishi naye hata kama yeye ananyanyasa au ni
hatari kwako. Kufanya hivi kungeendeleza hali ya dhambi ya mtu. Hiyo kwa hakika siyo kwa
faida yake, na wala kuendeleza hali ya dhambi hakutamtukuza Mungu. Inawezekana
kurekebisha mahusiano na kumpatanisha mtu—lakini kufanya hivyo kunakuhitaji juhudi ya
pamoja kati yako na mwingine katika upatanisho, siyo tu wewe kumsamehe kwa lile baya
alilofanya.
B. Msamaha unafafanuliwa: Msamaha ni uzoefu wa kihisia ambao unahusisha utu wetu katika ujumla
wake
1. Kila mtu ana utu ulio na mambo mengi ambao kwa kiwango cha chini angalau una sehemu kuu tatu
za asili yake (ukiongezea kwenye mwili). Hizo sehemu za mtu ni: (A) Uwezo wa ufahamu (nao ni.,
uwezo wa kufikiri, kuchambua, kujua, na kuelewa mambo); (B) Uwezo wa Utashi (nao ni., uwezo wa
kufanya maamuzi na kufanyia kazi hayo maamuzi; matumizi ya nia); na (C) Uwezo wa hisia (nayo ni.,
kipengele cha hisia; uwezo wa” kuhisi”). Kama lengo la msamaha ni kuondoa deni, msamaha“wa
kweli” na wa kudumu unaweza kutolewa tu ikiwa kutakuwepo na kuhusishwa kwa ukamilifu ufahamu,
hisia na utashi katika mchakato wa kusamehe.6
2. Kutokusamehe kunatokea wakati: (A) Kosa linatokea; (B) Tunaliona kosa kama maumivu au kwazo;
(C) Maumivu husababisha “joto” (ghafla) hisia za hasira na hofu(ya kuumizwa tena); (D) Baada ya
muda katika fahamu zetu tunakumbuka na kuishi katika (nayo ni., tunacheua) kosa, mkosaji na
makusudi yake, na matokeo ya kosa; (E) Hili linatupelekea kutosamehe, ambako kunahusisha “kupoa”
(kukawia, muda mrefu) hisia za chuki, uchungu, mabaki ya hasira, mabaki ya hofu, uadui, na msongo.
Hisia zenyewe ni zaidi ya “mihemko”; ni uzoefu wa mwili mzima unaohusisha ubongo, nyuroni, na
nyurokemikali, misuli, homoni, na njia nzima ya chakula.7
6
Worthington inaonyesha kwamba kuna msamaha aina mbili (au hata hivyo yaelezwa vizuri, namna mbili za kusamehe) (1)
msamaha kama uamuzi (“msamaha wa kuamua”— “kuachilia deni”); na (2) msamaha kama kuondoa maumivu ya ndani
(“msamaha wa mhemko”) (Worthington, 2003: ch. 2).
7
Hili na visehemu vidogo vinavyofuata viwili vipo kwa mujibu wa Worthington 2003: 30-45.
9
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
3. Kwa hiyo msamaha, siyo tu kufahamu na kutambua kwamba umekosewa na kuchagua kwa
kukusudia kuachilia na kuchukua hasara mwenyewe. Badala yake, msamaha ni tendo la kumaanisha
kutoka moyoni linalotambua kuwa kuumizwa isivyofaa na mtu mwingine kunasababisha maumivu ya
kihisia ya ndani yanayotuathiri katika utu wetu wa ndani. Msamaha ni “uzoefu wa kihisia” kwa sababu
ni kubalishwa kihisia. Msamaha unaondoa “hisia kali” (chuki, hasira, na woga), msamaha na “hisia
baridi” (kukwazika, uchunga, masalia ya chuki, masalia ya hofu, ukatili, na msongo ambao ni matokeo
ya kucheua kosa), kwa kubadilishana na “hisia chanya” kama vile upendo usio na ubinafsi, huruma na
rehema kwa mkosaji.8 Hii pekee “msamaha wa kihisia” kwa hakika “huponya moyo” (Worthington
2003: 44-45).
4. Tunaposamehe, tunaruhusu shauku ya kuzuia kulipa au kutafuta kumlipa kisasi mkosaji. Badala yake,
msamaha hulipa jema kwa baya. Msamaha huyaondoa mawazo yasiyofaa, na mawazo yanayomtakia
mabaya mkosaji na kuachilia mawazo yanayomtakia mema mkosaji. Hivyo, msamaha kwa hakika ni
karama ambayo inabeba neema, upendo, na uhuru (huru kutoka utumwa wa chuki, hasira, hofu, mawazo
mabaya, kuishi kwa mambo yaliyopita, kukaa kwenye makosa na maumivu). Tunatambua ya kwamba
mkosaji hana haki kwa mambo hayo (kama vile ambavyo na sisi hatuna haki ya kusamehewa na
Mungu).
5. Huwezi kisaikolojia ukapata uzoefu wa msamaha wa kweli—hata kama umesamehewa kweli-hadi
hapo hisia zinapobadilika. Hata kama ukibadilisha fikra zako, mapenzi yako, na matendo yako, hutapata
uzoefu wa msamaha mpaka hisia zako zibadilike—lakini kubadilisha fikra zako mapenzi yako, na
matendo yako lazima yakuongoze kufikia kubadilishwa kwa hisia zako. “Msamaha hautaondoa
kumbukumbu zinazoumiza; unaondoa hisia hasi” (Ibid.: 133).
6. Msamaha ni fumbo, kitu kama “ni heri kutoa kuliko kupokea” (Matendo 20:35) au“akupigaye shavu
lako la kuume mgeuzie la pili pia” (Math 5:39-42; Luka 6:29-30). Kwa msamaha tunatambua
kwamba: (A) kosa lilitokea ni baya na halikubaliki na siku zote litabaki kuwa baya na lisilokubalika: (B)
tuna haki ya kimaadili ya kuwa na hasira; lakini (C) kwa hiari yetu tunaachilia hiyo “haki” yetu kama
tendo la rehema na upendo, kama zawadi kwa mkosaji asiyestahili, kwa kumtii Kristo. Kwa hiyo
fumbo: kuwa huru mbali na hasira na kukwazika, kunampa mtu aliyekukosea zawadi ya msamaha na
kukuweka huru wewe mwenyewe.
8
Smedes anaweka hivyo hivyo; misingi ya msamaha inahusisha hatua tatu: “[1] Tunatambua ubinadamu wa mtu
aliyetuumiza sisi. [2] Tunatoa haki zetu ili kuzipata hata zaidi. [3] Tunafanya hisia zetu ziwe katika mtazamo wa Yule
tunayemsamehe.” (Smedes 1996: 6-12)
9
Sehemu hii kwa ujumla ni kwa mujibu wa Jeffress 2000: 57-58; Smedes 1996: 65-69; na Sande 2004: 20, 34.
10
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
kutatua tatizo kwa njia inayojenga. Tunapokumbuka msamaha wake na kukaribia uwezo wake,
tunaona vitu kwa wazi zaidi na kwa namna tofauti na tunaitikia katika migogoro kwa hekima
zaidi. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kupata suluhisho bora zaidi kwa matatizo yetu. Wakati huo
huo tunaweza kuwaonyesha wengine kwa hakika yupo Mungu anayefurahia kutusaidia sisi
kufanya vitu ambavyo tusingeweza kuvifanya wenyewe.” (Sande 2004: 20)
b. Sande anaelezea vidokezo vya kivitendo vinavyomfanya mtu aweke mtazamo wake kwa
Bwana: “Moja ya njia bora zaidi ya kuweka mtazamo wako kwa Bwana ni mara zote kujiuliza
maswali haya: Nitawezaje kumheshimu na kumpendeza Mungu katika hali hii? Kipekee, kwa
namna gani nitamsifu Yesu kwa kuonyesha kuwa ameniokoa na ananibadilisha? Kutafuta
kumpendeza na kumheshimu Mungu ni dira yenye nguvu sana kwenye maisha, hasa wakati
tunakutana na changamaoto ngumu. Yesu mwenyewe aliongozwa na malengo haya [tazama
Yoh 5:30; 8:29; 17:4]. . . . Wakati anaweka wazi utajiri wa upendo wa Mungu na kumpendeza
yeye kuwa muhimu zaidi kuliko kushikamana na mambo ya kidunia na kujipendeza
mwenyewe, kuitikia kwenye migogoro kwa neema, kwa hekima na kwa kuwa na kiasi inazidi
kuwa jambo la kawaida. Mtindo huu humpa Mungu utukufu na kuweka msingi wa upatanisho
wenye mafanikio.” (Sande 2004: 34)
10
Sehemu hii kwa ujumla ni kwa mujibu wa Jeffress 2000: 50-57; Smedes 1984: 125-51; na Smedes 1996: 55-74.
11
Ni kama hayati Mwigizaji wa Kiamerika, Buddy Hackett, alivyosema, “Mimi nimekuwa na mijadala michache na watu,
lakini hawana uchungu. Unajua ni kwanini? Wakati wewe una uchungu, wao wapo nje wanacheza.” (Jeffress 2000: 53)
11
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
kiwango cha hasira, kukua kwa ukomavu wa kihisia (McCullough 2000: 43-55; Witvliet, et al.,
2001: 117-23; Enright 2001: 45-67).
4. Kutokusamehe kunadhuru mahusiano yetu na wengine. Kwa kujifanya sisi wenyewe kuwa na
uchungu, watu walio na mioyo migumu, wanaojitazama wao wenyewe na ubaya tuliofanyiwa,
kutosamehe kunatutenga na watu wengine.
5. Kutokusamehe kunaathiri mahusiano yetu na Mungu. Dhambi, pamoja na dhambi ya kutosamehe,
inatutenga na Mungu (Isaya 1:10-15; 59:1-2; Mika 3:4). Kutengana huku na Mungu kunaathiri maisha
yetu katika dunia hii. Zaidi, kama anavyoeleza Carson: “Msisitizo [katika Maandiko] unaegemea
kwenye faida ya milele kwa kule kuishi sawa sawa na Mungu. Na katika nuru ya baadhi ya vifungu
(k.m., mfano wa mtumishi asiye mwaminifu ulionukuniliwa hapo juu), kuna hatari nyingi za binafsi na
za ndani za kutokusamehe wengine. Kwa maana hakuna, hakuna kabisa kilicho muhimu zaidi kama
kuhakikishiwa msamaha na Mungu.” (Carson 2002: 80)
6. Kusamehe kunawapasa watu wenye makosa kama sisi. Watu wengi si kwamba wao tu wanakosewa
sana, sisi si waathirika pekee. Lakini, sisi pia tunawakosea wengine; sisi pia tunawakwaza wengine.
Katika “ulimwengi halisi” kusamehe ni njia ya maisha—unapomwumiza rafiki wa karibu kwa njia ya
kumsema isivyo sahihi au kwa tendo (na sisi sote hufanya hivyo), rafiki yetu wa karibu ataumia na
kuachilia. Kwa hiyo, kufuta deni na kuachilia ni njia ya maisha. Maisha yasingewezekana kama watu
wasingekuwa wanasameheana kila wakati.
7. Kutokusamehe ni uchaguzi, kama vile ambavyo kusamehe ni uchaguzi. Tunabagua kuhusu nani
tumsamehe na nini tusamehe: tunasamehe tu maumivu “kidogo” na wale waliokosewa na watu wa
karibu nao. Hata hivyo, Yesu hakutupa hiari katika kuchagua maumivu, au watu, ambao tunatakiwa
kuwasamehe. Alisema tunapaswa kusamehe “hata saba mara sabini” (ambayo ni lugha ya alama ya
Yesu, kusema “bila mwisho” na wala siyo mara 490) (Math 18:22); tunatakiwa kuwapenda adui zetu,
siyo tu wale wanaotupenda sisi (Math 5:38-48). Yesu ni makali sana kwa wenye dhambi (kama sisi)
wanaokataa kusamehe wenye dhambi wengine, kwa sababu sisi sote ni wenye dhambi Smedes, anatoa
mtazamo wake katika mfano wa Yesu (Mathayo 18), anasema vema: “Yeye [Yesu] ni mkali kwa
sababu utata wa wenye dhambi kukataa kusamehe wenye dhambi kunashangaza ufahamu wa Mungu.
Hawezi kuchukuliana nayo; hakuna namna ya kiungwana ya kulichukuliana na hili. Kwa hiyo asema,
kama unataka msamaha wa Mungu na wewe unashindwa kumsamehe anayehitaji msamaha kidogo,
sahau kuhusu msamaha unaotaka. Ukiacha namna kiingereza cha King James kinavyosema, unapata
Yesu anasema kitu kama hiki: ukikataa kusamehe watu wengine wakati wewe unategemea
kusamehewa, unaweza kwenda motoni.” (Smedes, 1984: 150)
1. Vuta hisia ya maumivu. Ili kumsamehe aliyekukosea kwanza tunatakiwa kuwa wakweli kuhusu
12
Sehemu hii kimsingi ni kwa mujibu wa Worthington 2003: sura. 4-8; na, kwa upili, ni kwa mujibu wa Smedes 1996: sura
ya 15-20; na Enright 2001: sura ya 4-12.
12
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
tunapata kidogo tu ya kile tunachotarajia. Lakini tukisamehe tukilenga zaidi kupata, tunapata
tone tu ya faida. Ikiwa tutatoa zawadi ya msamaha kwa muhitaji mkosaji, ingawa, tunapokea
uhuru, amani, na pengine afya na kurejea kwa mahusiano. Msamaha hutoka kama maji kutoka
kwenye bomba. Unatusafisha. Unatuweka huru.” (Ibid.: 14)
b. Huruma hujitokeza katika hatua tatu: (1) Uelewa (i.e., unaelewa jinsi mtu mwingine
anavyoona mambo); (2) Kujilinganisha kihisia (i.e., unahisi na kufikiri pamoja na mtu
mwingine); na (3) Huruma (unahisi kuwa na huruma kwa ajili ya mtu mwingine, vile vile na
kumwelewa na kuwa na hisia sawa na yeye). Kupata msamaha wa kina, unaodumu, unahitaji
kufikia kina kirefu kuhurumia, kuhurumia kwa rehema.
c. Kuzingatia kweli kadhaa kutaongeza uelewa wetu wa, huruma yetu kwa ajili ya, mtu
mwingine: (1) “Hisia laini” (k.m., hofu, msongo, woga, na maumivu) mara nyingi hasira ya
ndani, ukatili, na kushambuliwa na mtu; (2) Watu wanashawishiwa na mazingira yao, hali na
nafasi; (3) Watu “wameunganishwa kwa nguvu” na usalama wao (na kwa hiyo huitikia ghafla
katika mambo yanayoonekana kama matishio kwao); (4) Watu wameathiriwa na uzoefu wa siku
zilizopita (wanaweza kuitikia kwa hofu na hasira sasa kwa sababu ya jinsi walivyokuzwa, au
uzoefu mwingine walioupitia zamani huko nyuma); (5) Watu mara nyingi huitikia kwenye
mambo bila kufikiria (hii ni kweli hasa wakati watu kihalisi, wanaitikia kutokana na kuumizwa,
kwa haki au kwa ubaya, na hali hiyo ikawa ni tishio kwao); (6) Tusisahau kamwe kwamba sisi
ni wakristo (na, kwa hiyo, kwa neema ya Mungu, na kutumia nguvu za Roho Mtakatifu,
tutaitikia kwa tendo au maumivu tuliyopata kutoka kwa mtu mwingine tukiweka mbali utu wetu
wa kale, tukiwa wakweli na wenye upendo na kuvaa “nia ya Kristo” ambaye sisi kwa hakika
tunayo nia yake (tazama Waef 4:15, 20-32; 1 Wakor 2:16).
d. Mbinu mbalimbali zinaweza kutusaidia kumhurumia mtu mwingine: (1) Omba kwa ajili ya
karama ya huruma; (2) Andika barua inayoeleza kana kwamba wewe ndiye Yule mtu
aliyekuumiza wewe, ukielezea misukumo ya mkosaji, mawazo na hisia alizonazo yeye; (3)
Andika barua ya kuomba msamaha kwa mtazamo wa mkosaji; (4) Ongea na kiti kitupu,
ukimwambia mkosaji unachofikiri na kuhisi, kana kwamba mkosaji ameketi kihalisia katika kiti
hicho-halafu fanya kinyume chake, kwa kukaa kwenye hicho kiti na kujiona kana kwamba
wewe ndiyo mkosaji, ukimweleza kile kilichokusukuma ufanye yale uliyofanya, na kuomba
msamaha kwa yale uliyofanya; (5) Ongea na rafiki au shiriki katika kikundi cha waumini
wenzako kusaidiana kuhusu mambo ya msamaha; (6) Fanya au tengeneza kitu fulani kuashiria
hisia zako za huruma kwa mtu mwingine; (7) Tafakari juu ya huruma za Yesu kwa watu kama
mtu huyo; (8) Omba kwa ajili ya huyo mtu mwingine [siyo moto wa mbinguni umwangamize,
lakini Mungu amkaribie, na kumbariki, na amgeuze na kumfanania Kristo, hata hivyo wakati
wewe unaomba hivyo hayo hayo yanatokea kwako]; (9) Tafakari kuhusu makosa yako
mwenyewe, udhaifu, jinsi ulivyoumiza, ulivyolaghai, ulivyotumia, ulivyodharau, upuuzaji, na
vinginevyo ulivyokwaza wengine.
3. Zawadi ya Msamaha isiyo na ubinafsi. Tafiti zinaonyesha ikiwa watu hawana rehema, kwa hakika
hawataweza kusamehe. Pamoja na hayo, hata baadhi ya wale wanaojenga huruma kwa ajili ya mkosaji
hawasamehi.
a. Wakristo wanahitajika kutafakari dhambi zao wenyewe zilizosamehewa na Mungu na watu
wengine waliowasamehe. Ili kupata uelewa wa kina wa ubinadamu wetu wenyewe na
unyenyekevu inafanya iwe rahisi kusamehe wengine waliotukosea. Kwanza kukumbuka
makosa yetu, kisha tutakumbuka uhuru wa kina na shukrani tulizokuwa nazo tuliposamehewa
mokosa yale. Shukrani na unyenyekevu ni matendo ya msingi ya ukristo yanayotufanya sisi
kuangalia mambo ya wengine.
b. Kutokuwa mbinafsi ni upendo unawaelekea wengine; ni kutoa bila kutegemea kupata kitu.
Moja ya zawadi kubwa tunazopokea ni zawadi ya kusamehewa—ni kuweka huru; ni kuinua;
inweza kuwa inabadilisha maisha. Ni zawadi ambayo Kristo ametupa sisi na ambayo watu
wengine wametupa sisi. Msamaha ni “nguvu kamilifu” ya upendo. Hivyo, ingawa chuki
inaweza ikatupa sisi “nguvu ya kitambo ya kuendeleza ukatili kwa siku ya leo . . . chuki haina
nguvu ya kudumu ya kuandaa hatima nzuri zaidi ya kulipa kisasi. Ni msamaha ndiyo unaotoa
chemichemi ya uponyaji ya kudumu kwa siku zijazo. Kwa mwendo mrefu msamaha una nguvu
kuliko chuki.” (Smedes 1984: 146) Mkristo mwenye kina ni mtu mwenye shukrani yenye kina;
mtu mwenye shukrani hawezi kusaidia bali zawadi ya msamaha ambayo imempatia faida
kubwa.
4. Toa msamaha hadharani. Unasamehe, kwanza na kwa umuhimu mkubwa, ndani yako mwenyewe—
14
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
moyoni mwako, katika ufahamu wako, na nafsini mwako; na kujitoa hadharani kusamehe baada ya
kuwa angalau umetoa “msamaha wa maamuzi,” kama siyo “msamaha wa hisia,” ndani ya moyo wako
mwenyewe na ufahamu.
a. Kujitoa hadharani kwa uamuzi ambao umefanya kibinafsi inasaidia kukazia uamauzi ule na
kushinda mashaka juu ya ama “umemsamehe sawa sawa” mkosaji, ambayo yanaweza kutokea
nafsini hapo baadaye, wakati unaporejea kufikiria juu ya mkosaji au tukio. Kujitoa kusamehe
hadharani, ni kama, kubatizwa au kushiriki meza ya Bwana—“ni ishara inayoonekana kwa nje
ya neema ya kiroho iliyomo ndani” ya msamaha uliokwisha kuutoa.
b. Kuna mbinu kadhaa ya kujitoa hadharani kusamehe: (1) Tiisha ufahamu wako
kutomdhalilisha mwenzako pale mawazo hasi yanapotokea (jiambie mwenyewe “achilia” ku-
“acha kutafuta kosa”; “badili maudhui katika ufahamu” wakati mawazo hasi yanapojiingiza).
Vivyo hivyo, tafakari juu ya, rudia, hata andika, mambo chanya ya huyo mtu mwingine.
(2) Weka ishara ya msamaha wako. Andika kosa kwenye mkono wako; kwa kuosha mara kwa
mara na kazi itafutika. Au, beba jiwe kubwa kwenye mkono wako ulionyoosha (kama lile “jiwe
la kwanza” ambalo Yesu alitoa mwaliko litupwe kwa mwanamke kahaba aliyefumaniwa [Yoh
8:7]); ona msongo na maumivu unayopata kama maumivu na msongo wa kutokusamhe—
wakati uzito wa ile shauku ya kulipa unapokuwa mkubwa kiasi kwamba hutaki kuendelea
kushikilia tena zaidi, achilia jiwe lianguke kutoka mkononi mwako kama ishara ya kusamehe
kwako. Au, andika kosa kwenye karatasi, na kisha choma kwa moto na sambaza majivu. Au,
andika kosa kwenye karatasi na upigilie kwa misumari kwenye msalaba wa mti, au iache
kwenye au chini ya msalaba kanisani kwako. Kwa kuyafanya haya yote, kumbuka kwamba pia
unatoa kutokusamehe kwako, na maumivu yako, kwa Yesu—yeye anajua anayabeba; huhitaji
wewe kuyachukua. (3) Andika kusamehe kwako. Andika rasmi “cheti cha msamaha” ambayo
utatunza ili kukuhakikishia nyakati za mashaka kwamba kwa hakika, ulishamsamehe kikamilifu
aliyekukosea. (4) Mwambie mtu mwingine kuhusu kusamehe kwako. Mwambie Mungu, wewe
mwenyewe, mwenzi wako, rafiki unayemwamini, mchungaji wako, watu hawa wote
watakusaidia nyakati za mashaka. (5) Mtendee mtu mwingine kana kwamba umeshamsamehe.
Kadiri tabia yako inavyokuwa njema, itakazia uamuzi wako wa kusamehe uliochukua na hisia
zako za huruma na upendo.
5. Tunza msamaha. Mawazo na hisia za kutosamhe zinaweza kuinuka ndani yetu (kama vile ambavyo
mawazo ya dhambi—tamaa, ulafi, kiburi, chuki, n.k.—vinavyoweza kuinuka ndani yetu). Kwa
kumwona Yule mtu, akiwa mahali fulani maalumu, kwa kusikia jambo fulani, tarehe ya maadhimisho,
na mambo mengine, au tunapokuwa tumechoka, wapweke, au tunapokuwa na msongo, yaweza
kusababisha mawazo na hisia zisizotakiwa za kutokusamehe kuinuka ndani yetu. Ni katika nyakati
kama hizi tunatakiwa kushikilia msamaha wetu ambao tulikwisha toa na ambao tuliutoa hadharani.
a. Kuna mbinu kadhaa zinazoweza kutusaidia kushikilia msamaha katika nyakati hizo: (1)
Tambua kwamba maumivu ya jeraha la kukumbuka siyo sawa na yale ya kutosamehe
(kutosamehe kunahitaji kucheua; usijiachilia kucheua kunakokusudia kulipa kisasi); (2) Usiishi
kwenye hisia hasi (Kwa kujishughulisha jitoe mwenyewe—imba, omba, msifu Bwana, fanya
kazi fulani ya kushughulisha viungo—kuliko kukaa katika mawazo au hisia zilizojaa maumivu
na chuki); (3) Jikumbushe mwenyewe kwamba ulishamsamehe yule mtu (na jikumbushe zile
nyakati ulipojitoa mwenyewe hadharani kusamehe); (4) Tafuta kujihakikishia kutoka kwa
mwenzi, mshirika au rafiki (mtu fulani uliyemshirikisha kusamehe kwako aweze kukusaidia
katika nyakati za mashaka au msongo); (5) Tumia kumbukumbu ulizoweka (soma “cheti cha
msamaha,” barua, au maandishi mengine uliyoandika yanayoweka kumbukumbu ya kusamehe
kwako); (6) Tazama tena, pitia kwa upya katika mawazo, na tendea kazi tena mtindo wa utoaji
wa msamaha.
b. Fanyika mtu wa kusamehe zaidi. Hii huchukua maisha yote, lakini inasaidia kukuumba na
kumfanania zaidi Kristo. Zaidi, kanuni ya kufanyika kuwa mtu wa msamaha zaidi inakusaidia
wewe kufanya “halisi,” na kushikilia, msamaha uliotoa kwa mtu fulani kutokana na kosa fulani
maalumu. Kuna kanuni kadhaa zitakazokusaidia kufanyika kuwa mtu wa msamaha zaidi: (1)
Fikiria kwa nini unataka kuwa mtu wa kusamehe zaidi Mwombe Bwana auchunguze moyo
wako: je misukumo yako ni ya kibinafsi, au kwa sababu unataka kuwa mtii na mwenye kiasi, au
una misingi ya shukrani, upendo na huruma? (2) Tambua majeraha yako makubwa ya huko
nyuma na samehe. Kadiri unavyoweza kusamehe makosa ya huko nyuma na kujifunza katika
hayo, ndivyo inavyozidi kuwa rahisi kwako kusamehe majeraha yatakayojitokeza siku zijazo.
(3) Samehe jeraha moja kwa wakati mmoja. Kazana kutoa msamaha wa kimaamuzi na wa
15
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
kihisia; kadiri unavyoendelea na muundo wa REACH, chunguza maendeleo yako ili kuonyesha
kwamba kuna maendeleo. (4) Tambua mashujaa wa msamaha. Kusoma kuhusu, au kuongea
kuhusu, watu waliosamehe sana inaweza kuwa na uvuvio zaidi na kututia moyo. (5) Jipime
mwenyewe. Kutokusamehe kunaweza kukawa tabia mbaya, kwa hiyo kuwa mwungwana
kwako mwenyewe na tunza “wajibu wa kusamehe.” (6) Punguza sifa mbaya na palilia haki.
Kwa kudhamiria kazana kuwa na haki zaidi ya kusamehe tu. Jielekeze kipekee si juu ya nini
cha kuepukwa kufanya tu bali lipi utafanya ili kuwa mtu mwenye haki zaidi. Kwa mfano, amua
ni tabia ipi utahitaji kujenga na kisha andika utakachofanya kudhihirisha tabia hiyo: k.m.,
“Kama ningekuwa na (upendo) zaidi ninge (tia moyo watu, ningejaribu kuwaelewa zaidi,
kuwasikiliza) mara kwa mara.” (7) Badilisha uzoefu wako uliopita. Tumia huruma yako na
waza kwamba Yesu anamtia moyo mtu aliyekuumiza. Hii itasaidia kudhania kwako na
kumbukumbu zako za maumivu ya tukio lililopita. (8) Weka mpango mkakati wa kujiendeleza
mwenyewe Jaribu kukabili maisha yako kwa kudhamiria na kidhamira, ukijipa muda wa
kutafakari na kuomba, kupanga na kupumzika.. Maisha yaliyolemewa na shughuli ni magumu
sana kuyatiisha, matokeo yake, msamaha wetu, huruma na upendo kwa wengine huwa vigumu.
(9) Fanya mazoezi ya kusamehe katika mazingira ya kinadharia. Kufanyia mazoezi msamaha
kabla kuhusu hali zinazoweza kujitokeza inaweza kukusaidia pale mazingira halisi yanayohitaji
msamaha yanapojitokeza. (10) Fanyia mazoezi msamaha siku kwa siku. Unapopanga shughuli
zako za siku, fikiria kuhusu watu utakaoshughulika nao siku hiyo. Waweke kwenye maombi, na
hali za kuumiza zinapotokea tumia ule mtindo wa kusamehe vilivyo. (11) Tafuta msaada kwa
mtu. Rafiki unaowaamini, wachungaji, na wengine waliofunzwa na wenye uzoefu katika
maandiko na katika stadi za kusamehe wanaweza kutoa ushauri wa kufaa na msaada. (12) Anza
kampeni ya kuwapenda adui zako. Au kibinafsi, au ni vizuri zaidi, ukiwa na kundi unalohusiana
nalo kanisani, omba, panga, na fanyia kazi mikakati kwa kufanya mema kihalisi kwa adui zako.
Uwe na juhudi katika kuonyesha upendo wa Kristo kwa wale wasiopendeka.
13
Hiki kisehemu kimsingi ni kwa mujibu wa Enright 2001: sura ya 11.
16
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
c. Mahusiano kati yako na mkosaji yamevunjika na pande zote mbili zina hasira. Upande usio
na hatia unaweza ukaanzisha mchakato wa upatanisho kwa kuomba msamaha kwanza, ambao
unaweza ukasababisha upande wa pili kuelezea masikitiko yake, ambayo yatafungua mlango
kwa wewe kutoa msamaha.
d. Kosa lilifanyika muda mrefu uliopita, na mkosaji si sehemu tena ya maisha yako. Fursa
inaweza isitokee ya kueleza msamaha kama huyo mtu amekufa, au hapatikani tena kwa sababu
zingine. Hata hivyo, unaweza ukaonyesha kusamehe kwako kwa ishara (kama ilivyoelezwa
hapo mapema), au ukaelezea msamaha wako kwa mwanafamilia ya mkosaji, ukoo, kabila au
kanisa au watu wengine wa kati ili kufanya kikao cha kusameheana.
e. Mkosaji hana wazo kwamba wewe umekwazika. Mtu anatakiwa alete hoja hiyo ya zamani
kiufundi sana; kama ilivyodokezwa mapema, unatakiwa kuzingatia kwamba inawezekana
kuanzisha mjadala wa jambo unaweza kuleta madhara zaidi au mema zaidi kwa mtu mwingine
vile vile na kwako mwenyewe.
V. Kujisamehe Mwenyewe14
14
Hiki kisehemu ni kwa mujibu wa Worthington 2003: 222-25; Smedes 1984: sura ya 8; Smedes 1996: sura ya 12; na
Jeffress 2000: 183-84.
17
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
B. Ingawa kujisamehe mwenyewe inawezekana ni vigumu zaidi kuliko kusamehe wengine ni lazima
kujisamehe mwenyewe inapohitajika kufanya hivyo
1. Kimsingi, Yule aliyekosewa ndiyo pekee kwenye mamlaka ya kusamehe aliyemkosea: “kujisamehe
mwenyewe” kunakuweka wewe katika majukumu mawili kwa wakati mmoja. Pamoja na hayo, mara
kwa mara tunajiweka juu zaidi kwa sababu hiyo hiyo: tunajicheka wenyewe; tunajidanganya wenyewe;
tunajipongeza wenyewe; tunajiumiza wenyewe; tunajilaumu wenyewe. Kwa nini pia tusijisamehe
wenyewe?
2. Tunaweza kujisamehe wenyewe kwa njia ile ile tunayotumia kuwasamehe wengine. Tunahitaji kuwa
wakweli kuhusu sisi wenyewe, kufahamu kosa tulilofanya, kuungama na kutubu dhambi (kugeuka
kutoka) katika njia zetu mbaya. Kwa hiyo, kujisamehe mwenyewe kwa namna Fulani ni tofauti na
kusamehe wengine bure hata wale waliotukosea waliokataa kutubu; kujisamehe wenyewe ni zaidi
Mungu kutusamehe sisi—kama vile Mungu anavyotusamehe sisi ni kwa ajili kurejesha mahusiano
sahihi kati yetu na Mungu, kwa hiyo msamaha wetu wenyewe ni kwa ajili ya kurejesha utimilifu wetu
(“mahusiano sahihi na sisi wenyewe”). Kwa hiyo, toba na kujutia ni muhimu katika kujisamehe
wenyewe.
3. Kama ilivyo aina nyingine ya msamaha, tunajisamehe wenyewe kwa mabaya matendo tuliyofanya,
matendo ambayo kwayo tunajilaumu wenyewe na ambayo kwayo tunastahili lawama, na siyo kwa
sababu ya sisi ni nani na vile “tulivyo.” Tunaweza kufuata mchakato ambao tulitumia kusamehe
wengine ili kujisamehe wenyewe. Zaidi, hakuna kuchelewa katika kujiambia mwenyewe “Mungu
amekusamehe wewe na hivyo nitajisamehe.” Tunaweza kurudia hayo kwa ajili yetu wenyewe wakati wa
mashaka yanapotokea. Tunaweza kuwahusisha wenzi wetu, wachungaji, au marafiki waaminifu ili
watusaidie katika kujisamehe wenyewe. Tunaweza kuigiza sehemu ya mtu aliyesamehewa, na kuacha
kujipiga wenyewe vichwani kwa jambo ambalo Mungu mwenyewe ametusamehe ambalo kwa hilo
tumefanya kila lililo katika uwezo wetu kujirekebisha na kutafuta msamaha kwa mtu tuliyemkosea.
4. Kujisamehe mwenyewe kunaweza kuwa na faida ya ziada ya kutupa sisi picha ya wazi zaidi ya asili
yetu ya kweli tofauti na Kristo. Mara zote tunaona ugumu kukiri kwamba tumefanya mabaya—wakati
mwingine kosa kubwa la kimaadili. Tunajidanganya wenyewe kwa kuamini kwamba sisi siyo kama
“watu wabaya” wanaoweza kudanganya, kusema uongo, kuiba, kubaka, kuua, au kufanya aina zote za
uovu. Tunapaswa kujua zaidi (tazama Math 5:21-32; Marko 7:14-23). Kukabiliana moja kwa moja na
uovu mioyoni mwetu kunatusaidia sisi kupata ukweli sahihi kuhusu sisi wenyewe, inasaidia kuondoa
kiburi chetu, na hutusaidia kuwa kwenye njia ya unyenyekevu. Kama vile ambavyo kusamehe wengine
kunaweza kuonekana kama “ishara ya nje na alama inayoonekena” ya ndani ya msamaha wa kiroho ule
ambao Kristo ametupa sisi, kwa hiyo kujisamehe wenyewe inaweza kusaidia msamaha wa Kristo kuwa
“halisi” kibinafsi na katika hisia.
A. Toba siku zote inahusika na mkosaji (yule anayepokea msamaha) siyo na mwathirika (yule anayetoa
msamaha)
1. “Toba” haihusishi siyo tu hisia za majuto kwa kosa lililofanyika lakini ni “badiliko la ufahamu” au
“kugeuka.” Kwa maneno mengine, toba ni kugeuka kutoka kwenye mwelekeo mbaya ili kufuata njia
sahihi (Zodhiates, ed., 1993: metanoéō; metánoia).
2. Na katika hatua yake kina sana, toba “maana yake ni kujuta kwa kumaanisha juu ya ukweli kwamba
ulichofanya ni kibaya kimaadili, bila kujali kwamba ni lazima au si lazima upate matokeo yasiyo
15
Sehemu hii kwa ujumla ni kwa mujibu wa Jeffress 2000: ch. 4; Worthington 2003: 51-52; Smedes 1996:sura ya 11; na
Smedes 1984: sura ya 7.
18
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
upatanisho na mtu huyo. Kama ilivyoelezwa hapo mapema: Inahitaji tu mtu mmoja
kusamehe; inahitaji watu wawili kupatana.16
c. Toba ni muhimu ili kurejesha nafasi: Hii ndiyo tafauti ya upatanisho. Ingawa kosa la mtu
binafsi dhidi yako, mtu binafsi, anatakiwa kusamehewa bila masharti, dhambi hizo zinaweza
kuwa na matokeo. Matokeo yake, ingawa unatakiwa kutendea kazi kwa kutumia mchakato wa
msamaha wa REACH kumsamehe mtu aliyeiba fedha zako, au aliyebaka binti yako, au
aliyekusababishia wewe maumivu mengine yoyote au jeraha, kumsamehe kwako yule mtu
hakumwondoi kwenye mkondo wa sheria kwa kitendo chake; kwa hakika, anaweza akapata
matokeo magumu (kuhukumiwa kifo, kufungwa, faini, fidia, aibu, kuondolewa kazini, n.k.) kwa
ajili ya kile alichofanya. Kwa hiyo, katika Math 18:15-20, 1 Wakor 5:1-5, na 2 Wakor 2:5-8
Yesu na Paulo wanaagiza kwamba washirika wa kanisa waliotenda dhambi wanatakiwa
kunidhamishwa (lakini hitimisho ni mchakato wa urejesho) na kanisa ikiwa dhambi zao
zimethiri kanisa.
d. Toba ni muhimu ili kumwondolea mtu hatia na aibu. Yote mawili aibu (uzoefu wa kibinafsi
na hisia za kutenda mabaya, kudhalilika, kutengwa) na hatia (kujua ukweli kwamba upo
kwenye kosa, na ni mkosaji) haitaanza kumwacha mkosaji mpaka atakapotambua, atakapokiri,
na kutubu hatia. Kisha anaweza akaanza mchakato wa kurejeshwa kwa watu na jamii
iliyotengana naye, aibu yake, pamoja na hatia yake, inaweza kupunguzwa au kuondolewa.
16
Hiyo inaweza kuwa ni sababu nyingine kwa nini Mungu anatutaka tutubu na kuunganisha na hali ya Yeye kutusamehe
sisi: msamaha wake kwa hakika hautuachi peke yetu, katika hali ya kusamehewa na pamoja na hayo kuwa nje ya
mahusiano na yeye; bali, msamaha wake huturudisha katika mahusiano sahihi na yeye. Hiyo inahusisha yeye kutuchagua,
kutufanya wana, kutukomboa, kutupa urithi na kutuweka muhuri kwa Roho Mtakatifu (Waef 1:3-14). Kama Smedes
anavyoeleza, “ikiwa watu wanataka kusamehewa na Mungu, wanataka kuunganishwa na yeye wakati huo huo. Lakini
Mungu anataka mwunganiko wenye uadilifu. Na toba siyo kitu kingine bali ni kuwa wakweli kuhusu kile tulichofanya
kuvunja mwunganiko wetu na Mungu. Hii ndiyo maana mtu hawezi kutarajia kusamehewa na Mungu mpaka pale
atakapotubu kwanza.” (Smedes 1984: 92-93)
Kina cha Mungu kutusamehe sisi-ambako kunahusisha kurejeshwa kwetu katika mahusiano sahihi na yeye-
imeelezwa kwa usahihi na Sande katika mazungumzo yake na mtu aliyekuja kutaka ushauri kwake, Rick, ambaye alikuwa
akipata ugumu wa kutoa msamaha kikamilifu (na kupatana) na mke wake, Pam (ambaye alifanya uzinzi): “Ninaweza kuona
kuchoka katika uso wake. “Mimi’nina hakika wote wawili mpo kwenye maumivu makali, Rick. Lakini sidhani talaka
itamaliza hilo. Ninyi mtakanyaga tu aina moja ya maumivu kwa lingine. Kuna njia ya kuweka ndoa yenu pamoja na
kuweka yaliyopita nyuma yenu kwa hakika. Lakini hautaipata kwa msamaha mtupu uliompatia Pam.”
“Unamaanisha nini, ‘msamaha mtupu?”
“Rick, fikiri kwamba ndiyo tu umeungamana dhambi yako mbaya sana kwa Mungu, na kwa mara ya
kwanza akasema na wewe kwa sauti: ‘Nimekusamehe, Rick, lakini siwezi kamwe kuwa karibu na wewe.’
Ungehisije?”
Baada ya ukimwa wenye mshangao, akajibu, Ninafikiri nitahisi inawezekana Mungu hakunisamehe mimi
kwa hakika.”
“Lakini hivyo si sawasawa na wewe unavyomsamehe Pam?” Nikauliza.
Rick akatazama kwenye sakafu, anahangaika kutafuta jibu.
Kwa sauti ya chini, nikaendelea, “Fikiria badala ya Mungu kusema, Rick, Nimekusamehe. Ninakuahidi,
kamwe sitafikiri kuhusu dhambi yako tena, au kuishi nayo au kutafakari juu yake. Ninaahidi sitaibua tena na
kuitumia dhidi yako. Ninaahidi sitasema na watu wengine juu yake.Na ninaahidi sitaruhusu dhambi hii isimame
kati yetu au kuzuia mahusiano yetu.”
Baada ya kimya kirefu machozi yakaanza kulenga machoni mwa Rick. “Ningejua nimesamehewa
kikamilifu . . . Lakini nisingestahili msamaha kama huo baada ya yale niliyomtendea Pam.”
“Je ungestahili tena kuupata?” Nikauliza. “Msamaha wa Mungu ni zawadi ya bure iliyonunuliwa kwa
ajili yako na Yesu kwa mauti ya msalaba. Hakupi msamaha kwa sababu umejistahilisha. Anakusamehe kwa
sababu anakupenda. Unapotambua thamani ya msamaha na jinsi ambavyo hatustahili, utahitaji kumsamehe Pam
kwa namna ile ile aliyokusamehe yeye.” (Sande 2004: 202)
Kwa hiyo kama ilivyofafanuliwa hapo juu, kama vile ambavyo ipo tofauti kati ya Mungu na mtu, vivyo hivyo
inaonekana tofauti kati ya msamaha wa kiungu na msamaha kati ya mtu na mtu. Pamoja na hayo kuna mpishano wa wazi
kati ya msamaha na upatanisho: Rick anaelewa asili ya msamaha wa Mungu ambao ulimwongoza yeye kumwomba
msamaha Pam kwa ajili ya uchungu na kukosa kumfurahia alioonyesha kwake pamoja na madai yake ya kuwa
“amemsamehe” yeye. (Kwa kutumia misemo ya Worthington, Rick mwanzoni alikuwa ametoa “msamaha wa kihisia”;
alipomwomba Pam amsamehe kwa ajili ya uchungu na kukosa kwake furaha, alikuwa amefikia hatua ya “msamaha wa
kihisia” vile vile.) Kisha, hilo lilimsababishia Pam afunguke na kueleza hatia yake mwenyewe, aibu, na hofu, na hatimaye
wakafikia kwenye urejesho wa ndoa (Ibid.: 203).
20
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
B. Maandiko hayahitaji toba kuwa masharti kwa ajili ya msamaha wa mtu kwa mtu
1. Vifungu kadhaa (k.m., Marko 1:14-15; 6:12; Luka 13:3; 24:47; Matendo 2:37-38; 1 Yoh 1:9)
vinaunganisha msamaha na toba. Ingawaje, mazingira hayo yote yanajadili msamaha wa Mungu,
wokovu, na kurejeshwa kwa mwenye dhambi katika mahusiano yake sahihi na Mungu. Hakuna hata
moja kati ya mistari hiyo inayodai mkosaji atubu kwanza kabla hajasamehewa katika mazingira ya
msamaha wa mtu na mtu. Zaidi, hiyo yote inajihusiana na watu wanaotaka kusamehewa, siyo na watu
wanaohitaji kufanya jukumu la kusamehe.
2. Vifungu viwili pekee, wakati mwingine vimedai kufanya toba kuwa masharti kwa ajili ya msamaha
wa mtu na mtu: Math 18:15-20 (“Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye . . . na asipolisikiliza
kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru”); na Luka 17:3-4 (“Jilindeni; kama
ndugu yako akikosa, mwonye;akitubu msamehe. Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na
kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe”). Wakati mwingine mfano wa mwana
mpotevu, Luka 15:17-21 (“Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako
tena.”), inanukuliwa vile vile. Katika hayo matukio hakuna hata mmoja, pamoja na hayo, linalomhitaji
mkosaji kutubu kabla hajasamehewa:
a. Mtu analazimika kutofautisha kwa uangalifu kati ya nini kinaelezwa na nini kimeagizwa.
Luka 15 na 17 inaeleza mazingira ambayo mkosaji alitubu. Maandiko hayo hayasemi kwamba
mtu aliyekosewa anatakiwa kusamehe “kama, lakini kama tu” mkosaji atatubu. Vile vile,
hayasemi kwamba mtu aliyekosewa hatakiwi kusamehe kama mkosaji hajatubu.
b. Katika Luka 15, ona kwamba, ingawa mwana mpotevu “alizingatia moyoni mwake” na
akaelezea toba yake, baba alidhihirisha msamaha wake hata kabla ya mwana kutamka maneno
yake ya toba kwa baba (Luka 15:20).17 Angalia pia baba katika mfano huo alidhihirisha
misamaha yote miwili “msamaha wa maamuzi” na “msamaha wa kihisia” (Worthington 2003:
53-54).
c. Muktadha wa Mathayo 18 kimsingi unaonekana kuhusisha kisa cha marudi katika kanisa,
dhambi inayoathiri kanisa, na/au kurejeshwa kwenye ushirika au nafasi ya uongozi.
Ellingworth anaeleza kwamba nukuu ya Yesu katika Yoh 20:23 “kwa hakika ni kwa ajili kuleta
nidhamu katika jamii ya waaminio, na siyo kukataa kusamehe makosa ya mtu binafsi,” na Math
16:19 na Math 18:18 “zinafana, lakini bila shaka inarejea kiujumla kuhusu maamuzi ya nini
kinaruhusiwa na kukatazwa kati ya jamii kuliko msamaha peke yake” (Ellingworth 1992: 242).
Kama ni hivyo, msamaha ni wa thamani, ni lazima, na ni sehemu ya muhimu katika mchakato
wa urejesho. Tofauti kati ya hilo na binafsi, msamaha wa mtu kwa mtu imeonyeshwa na
kifungu cha karibu kinachofuata, ikianzia katika Math 18:21, mahali Petro ameuliza “Bwana,
ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?” Kristo hakuwa na haja
kwamba mkosaji atubu kwanza kabla ili asamehewe “hata saba mara sabini” (Math 18:22).
d. Hatimaye, sisi ni lazima tutambue katika fahamu zetu tofauti iliyopo kati ya kutoa msamaha
na kupokea msamaha.. “Jambo la kutubu ni muhimu sana ili kupokea msamaha, lakini haina
umuhimu wowote katika kutoa msamaha” (Jeffress 2000: 73). Luka 15 na 17 inaelezea habari
za watu waliohitaji kusamehewa; walielezea toba yao kama sehemu ya kupokea msamaha.
C. Msamaha hauwezi “kununuliwa” kwa toba, lakini msamaha usio na masharti unadhihirisha uhalisi,
nguvu, uhuru, heshima na upendo
1. Wengi hudhani kwamba “kama mtu aliyetukosea hatatubu, hastahili kusamehewa.” Smedes anajibu
hili kwa msisitizo mkubwa: “Kwa hakika, hastahili kusamehewa. Hakuna anayestahili. Na wala
machozi yote katika bahari ya Neptune hayawezi kumpa haki au kumfanya astahili. Msamaha katika
mazingira yoyote ni kwa ajili ya wale tu wasiostahili. Kuhuzunika kwa ajili ya makosa tuliyofanya
hakutupi haki ya kusamehewa. Inawezaje? Hakuna kitu cha aina hiyo yaani haki ya kusamehewa.
Msamaha hushuka tu kutoka kile ambacho wanatheolojia wanakiita neema-isiyogharimiwa, kibali
usichostahili. Neema iliyogharimiwa siyo neema hata kidogo. Kwa njia isiyo sawa, ikiwa tunastahili
kusamehewa, tusingeuhitaji.” (Smedes 1984: 90-91)
2. Siku zote kuna upungufu kati ya kile anachodai aliyeumia na kile ambacho mkosaji anaweza kulipa.
Katika kisa cha mwana mpotevu (Luka 15) hata baada ya mwana kusema, “Baba, Nimekosa,” hakulipa
17
Kwa kiwango hicho kwamba baba katika mfano wa Baba yetu wa Mbinguni, toba ni lazima kama ilivyojadiliwa huko
nyuma. Hata hivyo, ona kwamba ni baba ndiye aliyeanzisha kwa kukimbia kukutana na mwanaye, hata wakati mwanaye
“alipokuwa angali mbali.” Vile vile, Baba yetu wa mbinguni ndiye aliyeanzisha katika kutuokoa sisi. Tazama, kwa mfano,
Yoh 1:12-13; 6:37, 44; Waef 2:8-9.
21
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
fedha alizochukua au miaka ya kuumwa moyo aliyosababisha; kwa hakika, mwana alishatumia vibaya
urithi wake unaomwangukia. Hata toba ya kweli kabisa ya mbakaji haitarejesha ubikira uliopotea; toba
ya kweli ya mwuaji haitarejesha uhai; toba ya kweli ya mtu aliyeng’oa jicho lako haiwezi rejesha kuona
kwako. Toba haiwezi “kuvuka viwango”; ni upungwani kufikiri kwamba inaweza. Kwa hiyo siyo sahihi
kudai mkosaji atubu kabla hujamsamehe.
3. Huwezi kumfanya mtu yeyote atubu mahali popote. Mkosaji anaweza akawa amekufa, au
ameondoka, hawezi kutubu, ikiwa hafahamu kama amekukosea wewe, au tu hajali. Msamaha bila
masharti huzingatia hayo. Haifanyi msamaha wako umtegemee mtu fulani atubu jambo ambalo lipo juu
ya uwezo wako.
4. Msamaha usio na masharti ni kufanyia kazi mamlaka. Inakuweka wewe kwenye nafasi ya kuamua
kutoa au kutotoa msamaha wewe mwenyewe. Kuhitaji mkosaji atubu kabla ya wewe kumsamehe
kunakushusha wewe kwake. Kibaya zaidi, hilo linakufanya wewe umtegemee yule aliyekuumiza.
Kuhitaji mkosaji atubu kwanza kabla ya wewe kumsamehe kunampa mkosaji nguvu ya kutawala moyo
wako, ufahamu, na nia yako.
5. Msamaha usio na masharti unakuweka huru wewe dhidi ya mkosaji. Unakuweka wewe huru dhidi ya
kufungwa kwenye yaliyopita, uovu, maumivu, na ubaya. Unakuweka huru kutoka kwenye hali
tegemezi. Unakusaidia wewe kupona na kuendelea na maisha yako.
6. Msamaha usio na masharti huonyesha heshima kwa mtu mwingine. Kumsamehe mtu bila kumtaka
atubu kwanza kunadhihirisha kwamba unamwona yeye kama mtu mwenye uwezo wa kubadilika.
Inaweza kwa hakika kumpa motisha ya yeye kubadilika.
7. Msamaha usio na masharti ni kiwango cha juu cha kuonyesha upendo. Kama ilivyojadiliwa mapema,
moja ya funguo “hisia kali” ambayo inasababisha kutosamehe ni hofu. Na bado Biblia inasema
kwamba, “hamna hofu katika pendo; bali upendo wa kweli hutupa hofu njema” (1 Yoh 4:18). Kama
asemavyo Jeffress: “ikiwa toba ni hitaji ili kutoa msamaha basi hiyo ina maana kwamba ni lazima
tukutane na kila mtu aliyetukosea kabla ya kumsamehe kikamilifu. . . . Lakini tunataka kweli kutumia
maisha yetu kutafuta kuombwa msamaha kutoka kwa kila aliyetuzunguka? Tunataka kuwahakikishia
watu wawe wanakimbilia milimani wanapotuona tukiwaendea kama kila wakati tunataka ‘kuongea
kuhusu jambo binafsi? Na kwa umuhimu zaidi, je maisha hayo ya kukabili watu kwa namna hiyo
hayapingani na mantiki ya upendo wa kikristo, upendo ‘ambao hauweki kumbukumbu ya makosa’ (1
Wakor 13:5 NIV).” (Jeffress 2000: 80)
8. Msamaha usio na masharti hufuata mfano wa Kristo. Yesu alitusamehe sisi hata kabla hatujatubu
dhambi (tazama Marko 2:3-12; Luka 7:36-48; 23:33-34; Yoh 8:1-11). Kwa hiyo, tunapaswa kuwa
tayari kusamehe hata kabla hatujaombwa msamaha.
VII. Kupokea msamaha kwa ajili ya dhambi zetu tulizomkosea Mungu na watu wengine
18
Sehemu hii ni kwa misingi ya Jeffress 2000: 143-55 Smedes 1996: sura ya. 8, 14; na Worthington 2003: sura ya 3.
22
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
19
Namna moja yenye msaada sana ya kufikiri kuhusu msamaha wa wengine ni namna ambavyo Katekisimo ya
Waangalikana katika Kitabu cha Maombi ya Pamoja kinavyoelezea sakramenti: “Sakramenti ni alama ya nje nay a wazi ya
neema ya kiroho ya ndani, inayotolewa na Yesu Kristo kama hakikisho la kweli ambalo kwa hilo tunapokea neema hiyo”
(Kitabu cha Maombi ya Pamoja 1979: 857). Huo mtazamo wa kusamehe wengine kwa hakika umeanzishwa na maonyo ya
Kristo kuhusu mwunganiko wa msamaha wa mwanadamu na wa kiungu katika Math 6:9-15; 18:21-35; Marko 11:25-26;
na Luka 7:36-50.
20
Sehemu hii ni kwa mujibu wa Jeffress 2000: 155-64; Enright 2001: sura ya 14; na Chapman and Thomas 2006: passim.
23
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
ajili ya tulichofanya? (C) Je tukio hilo linajirudia rudia katika fahamu zetu (labda
tunapojaribu kulihalalisha)? (D) Je tunajilinganisha wenyewe na mtu tuliyemwumiza
(pengine tunajiambia wenyewe, “yeye ni mmbaya kama mimi nilivyo—au mmbaya
zaidi!”)? (E) Tumesema uongo ili kufunika tulichofanya kwa ajili ya aibu? (F) Maisha
yameathirikaje kutokana na kile tulichofanya (hata kwa yale “madogo” njia za
kutufanya sisi kuwa zaidi “wakali” au “wenye mioyo migumu”)? (G) Je tunalilia kuwa
huru kutoka kwenye aibu na hatia ya makosa yetu? (H) Tumeshakiri dhambi zetu kwa
Mungu na kupokea msamaha wake (na kwa namna hiyo, ndivyo tunavyopaswa vile vile
kutafuta msamaha kwa wale tuliowakosea)?
(3) Katika kisa cha mtu ambaye hajui matendo yako (kama vile mahusiano ya uzinzi na
mtu fulani, ingawa mwenzi wako hajui) inaweza kuwa mtego. Jeffress anapendekeza
angalau maswali matatu ya kujiuliza katika kisa hicho: (A) Je malipizi ni lazima?
Ikiwa upande mwingine umepata hasara, na haujui ni nani amesababisha hasara hiyo, ni
wajibu wako siyo tu kuomba radhi na msamaha bali na kufidia hasara; na kwa hakika
kufidia hasara kutadhihirisha nia yako ya kuomba radhi na ya kutaka msamaha.
(B) Kuna uwezekana gani kwamba kosa lako litajulikana? Uhusiano wa miaka
thelathini iliyopita unaweza usijulikane katika ndoa yako sasa, wakati huo huo uhusiano
wa miezi sita iliyopita unaweza ukajulikana kwa mwenzi wako, na kusikia habari
kutoka kwa mtu mwingine inaweza kuwa inaumiza zaidi kuliko kusikia kutoka kwako.
(C) Je kukiri kwako kutasaidia au kutaumiza upande mwingine? Anaongeza, “Hili ndilo
jambo la-msingi. Wakati mwingine shauku yetu ya ‘kukiri’ inaweza kuwa kwa ajili
yetu wenyewe zaidi. Wakati sisi tunaweza kujisikia huru kwa kupakua uchafu wetu
kwa mwenzi wetu, yeye anaweza akapata mshtuko. Wakati mwingine upendo wa
kujitoa dhabihu unatugharimu utayari wetu wa kubeba mzigo yetu wenyewe bila ya
kumwomba mtu mwingine kutusaidia mzigo.” (Jeffress 2000: 158-59)
b. Kuomba msamaha.
(1) Kumbuka kwamba “kuomba msamaha ni kumwomba mtu uliyemkosea afanye kitu
fulani: kukufungua wewe kutoka kwenye deni lako” (Jeffress 2000: 161). Kuomba
kukutana na mtu ni njia inayokubalika ya mawasiliano—kuongea na mtu mwingine ana
kwa ana inamsaidia mtu mwingine kusikia hali ya sauti, kupata maelezo ya lugha ya
viungo, na mwonekano wa usoni na kuuliza maswali ya ufuatiliaji, yote (au mengi) ya
hayo yanazuiwa na mazungumzo kwa njia ya simu au barua.21 Zaidi, kukutana ana kwa
ana inasaidia kuonyesha kujaliwa kwa tukio, na kwa hiyo kuonyesha ukweli wa shauku
ya kutaka msamaha. Hiyo hasa ni kweli kama, kwa sababu ya umbali utakaotembea au
mazingira mengine, itakugharimu kukutana ana kwa ana. Kama Jeffress anavyoeleza,
“Muda na kujitoa kunakohitajika kwa ajili ya juhudi hiyo inaweza kuwa kubwa, lakini
siyo kitu ukilinganisha na furaha ya dhamiri safi” (Ibid.).
(2) Kuomba msamaha kunahusisha zaidi ya kusema tu bila ya kufikiria, “Nisamehe.”
Inahusisha kukubaliana na maumivu ya kushushwa kunakotokea tunapokiri kwamba
tulikuwa na makosa. Hilo linaweza likawa gumu zaidi wakati mtu fulani aliye na
mahusiano ya kimamlaka (k.m., mume, mzazi, au mwajiri) analazimika kujinyenyekeza
na kuomba msamaha kwa mtu fulani anayemtegemea kwa karibu au mshirika
(k.m.,mke, mtoto, au mwajiriwa). Hata hivyo, “Tukitaka kuwa huru, ni lazima
tukubaliane na maumivu pamoja na huko kushushwa” (Enright 2001: 254).22
(3) Jeffress anaeleza namna nne za kumwomba mtu msamaha: (A) Kataa kulaumu.
Hata kama upande wa tatu, au hata mtu ambaye unamwomba msamaha, kwa kiasi
kikubwa ndiye aliyesababisha mgogoro, unatakiwa kujikita kwenye kosa lako
mwenyewe. (B) Tambua kosa ulilofanya. Usijaribu kupunguza ukubwa wa kosa
21
Kunaweza kukawa na utaratibu wa kipekee katika kila tamaduni au jamii wa kupanga kikao cha msamaha, kama vile
matumizi ya ndugu wa familia, wazee wa kijiji, viongozi wa ukoo au kabila, viongozi wa kanisa, au wengine kama “watu
wa katikati” au wawezeshaji. Kanisa lina wajibu wa kufanya au kujenga katika kusababisha msamaha.
22
Tunapaswa kukumbuka (na kupata kutiwa moyo na) hili: Sisi kuwa watiifu kwa kristo. Zaidi, Kristo alipata uzoefu wa
kuaibika hadharani na kushushwa kwa kudhihakiwa,kupigwa, na kusulubiwa uchi kwa dhambi ambazo watu wengine
walifanya; tunapomwomba mtu mwingine msamaha, tunapata tu kushushwa kibinafsi (labda tukiwa tumetenda dhambi
kosa kwa jamii, ambapo ukiri wetu ni lazima uwe kwenye hadhara) kwa sababu dhambi tuliyofanya sisi kwa mtu binafsi.
Kweli, “mtumwa si mkuu kuliko bwana wake” (Yoh 13:16; tazama pia Math 10:24; Luka 6:40; Yoh 15:20).
24
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
ulilofanya au kuongea kiujumla tu. Mwenzako anajua ulichofanya; sasa yeye anataka
kujua kama wewe unajua kikamilifu kosa lako. (C) Tambua maumivu uliyosababisha.
Mwenzako anataka kujua kwamba wewe unaelewa maumivu aliyoyapata kutokana na
matendo yako. Kutambua kwako hilo (au hata kusema huwezi kuamini maumivu [au
uchungu au usumbufu] ambao jambo hili limekusababishia”) itamfanya mwenzako awe
tayari zaidi kukusamehe wewe. (D) Mwombe mwenzako akusamehe. Usikiri tu kosa
ulilofanya kirahisi, bali hitimisha mazungumzo yako kwa kumwomba mwenzako kwa
hiari akuachilie katika madai aliyonayo dhidi yako yanayotokana na kosa lako. Huwezi
kudai msamaha; wala usitake kwamba eti mtu akusamehe wewe kwa ajili ya faida yake
mwenyewe. Badala yake, Jeffress anashauri kuomba msamaha kwa kusema kitu kama:
“Nimetambua kwamba nimekukosea kwa______. Nitafanya kwa kadiri niwezavyo ili
kwamba kamwe nisirudie kufanya hili, ingawa ninatambua siwezi kufuta maumivu
makubwa niliyokusababishia. Nilichofanya ni kosa, na simlaumu mtu yeyote ila mimi
peke yangu. Leo ninakujia wewe kuomba ikiwa nitapata nafasi moyoni mwako ya
kusamehewa kwa kile nilichofanya.” (Jeffress 2000: 163)
(4) Chapman na Thomas wanafuata muundo wa aina hiyo hiyo wenye hatua-tano kwa
ajili kudhihirisha kusikitika kwako na kuomba msamaha: (A) Eleza majuto yako (kwa
mfano., “Nisamehe.”); (B) Kubali kuwajibika (kwa mfano., “Nilikosea.”); (C) Fanya
malipizi/toa fidia (kwa mfano., “Nifanye nini ili kuweka sawa.?”); (D) Fanya toba ya
kweli (kwa mfano., “Mimi’ nisitende hivyo tena.”); na (E) Omba msamaha (kwa
mfano., “Tafadhali, utanisamehe mimi,?”) (Chapman na Thomas 2006: passim).
(5) Sande ana kanuni yenye hatua saba, amabayo anaiita “A saba za Kuungama”: (A)
Ongea na kila mtu aliyehusika. Kiri makosa yako kwa kila mtu aliyeathirika moja kwa
moja kutokana na kosa lako; (B) Epuka maneno, Kama, Lakini, na Labda. Neno
“kama” (n.y., “Mimi’ nisamehe kama nimefanya kitu fulani cha kukuhuzunisha
wewe.”) linaharibu ungamo lako kwa sababu linaonyesha kwamba wewe hujui kama
umefanya au hujafanya kosa. Vile vile, kitu kama yawezekana nilikosa,” labda
ningejaribu kutumia bidii zaidi,” “Nisingeshindwa kuzuia hasira yangu, lakini
nilichoka,” na “Mimi’ ninaomba nisamehe, nimeumiza hisia zako, lakini ulinihuzunisha
sana,” kiondoa uzito wa sehemu iliyosalia ya “ungamo” na inaharibu uwezo wa
kuwasilisha toba ya kweli; (C) Kiri jambo mahususi. Kadiri unavyoeleza kwa kina na
kimahususi wakati unaungama, ndivyo inavyokuwa rahisi kupata mwitikio chanya; (D)
Tambua Maumivu—Unahitajika kuonyesha kwamba unatambua vile ulivyomwumiza
au ulivyomwathiri mtu mwingine; (E) Kubaliana na Matokeo. Kukubali kwa uwazi
kupokea matokeo ya matendo yako, ikiwa ni pamoja na kufanya malipizi, inadhihirisha
toba ya kweli; (F) Badili Tabia Yako. Mwambie mtu yule uliyemkosea vile
ulivyojipanga kubadilisha tabia yako kwa siku za mbeleni; (G) Omba msamaha (na Toa
Muda). Ukiwa umefanya kwa makini hatua hizo hapo juu, unaruhusiwa kuomba kwa
wazi kusamehewa. Kuomba msamaha kunahamisha wajibu kwa mtu mwingine kuanza
mwendo unaofuata. Hata hivyo, mtu asimshinikize mtu mwingine kufanya uamuzi wa
haraka. Mtu aliyekosewa anaweza kuhitaji muda wa kufikiri, kuomba, na “kuchakata”
kosa na ungamo. (Sande 2004: 126-34)
(6) Inawezekana ikawa tunatafuta msamaha wa mtu ambaye ameshafariki, hayupo tena,
au amekataa kuongea nasi. Au, mtu anaweza akaitikia ombi lako la msamaha kwa
kutofautiana, kwa namna hasi, au hata kikatili. Ingawa hiyo ni bahati mbaya, kama
tukiwa wakweli na makini, kufanya yote katika kujuta, na kukubali kuwajibika kwa
tulichokifanya na kufanya malipizi, tumetubu (tumebadilisha njia zetu), na kutafuta
msamaha na kumaliza, bado sisi tunaweza kuwa na dhamiri safi kwa “kujua kwamba
hata Mungu au mwingine yeyote anaweza kukutuhumu tu kwa kosa ambalo
hatujajaribu kulirekebisha” (Jeffress 2000: 164).
c. Kukua katika Kristo, na kuwa mtu mzuri zaidi, kama matokeo ya uzoefu wako.
(1) Enright anashauri kwamba, kama matokeo ya makosa yetu na kutafuta kwetu
msamaha, tunatakiwa: (A) Tafuata maana katika makosa na kushindwa (mafanikio yetu
mara chache hutufundishwa sisi ukilingalinganisha na makosa yetu); (B) Tambua
kwamba sisi tuna nguvu kwa sababu ya kile tulichopitia (kwa sababu ya ujasiri
unaohitajika kukiri kosa na kumkabili mtu tuliyemwumiza, tutakuwa imara na wenye
uwezo zaidi kukabiliana na makosa ya siku zijazo bila hofu); (C) Tambua kwamba
25
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
hatupo peke yetu (n.y., tunaweza kuhitaji msaada katika mchakato huu,23 na tunatambua
kwamba sisi ni kama watu wengine—hatutakuwa tena wenye kiburi na wenye
kudhihaki wengine); (D) Fanya maamuzi, na chukua hatua za lazima, za kutorudia
kosa; na (E) Pokea uhuru kutoka kwenye hatia, majuto, na aibu ambao huletwa na
kukiri kosa na kupokea msamaha. Mambo haya yote yanatakiwa yatulete sisi karibu na
Kristo na kutufanya tufanane na Kristo zaidi.
(2) Kwa kupitia Mambo yale yale matano ambayo Enright anayoshauri tunagundua
baada ya kupokea msamaha yanapatikana kwetu kama, bila kosa letu wenyewe, mtu
mwingine hawezi au hataweza kutusamahe. Kama tukitimiza wajibu wetu, uhuru na
ukomavu unaotokana na kuomba msamaha, malipizi na kutubu havikaniki kwa sababu
mtu mwingine baki hawezi kujiletea msamaha yeye mwenyewe.
(3) Sande anashauri kwamba tunaweza kupata uhuru kutoka kwenye dhambi zetu kwa
“ku[fanya] kazi pamoja na Mungu ili atubadilishe mitazamo [yetu] na tabia huko
mbeleni” (Sande 2004: 134). Anadokeza kwamba Mungu anataka kutusaidia tukue na
kubadilika na kwamba hakuna dhambi au tabia katika maisha yetu ambayo hatutaweza
kuishinda kwa neema yake. Wajibu wetu ni: (A) omba; (B) kujifurahisha wenyewe
katika Bwana; (C) kujifunza; na (D) kuweka kwenye vitendo yale tunayojifunza (Ibid.:
134-35).
UPATANISHO
I. Mungu ametupatanisha sisi na nafsi yake mwenyewe na kutupa huduma ya upatanisho (2 Wakor 5:16-
21): 16 Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua
Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena. 17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo
amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. 18 Lakini vyote pia vyatokana na Mungu,
aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho, 19 yaani, Mungu alikuwa
ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu
neno la upatanisho. 20 Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu;
twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. 21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi
kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.24
II. Mungu amemaliza vikwazo vyote vinavyozuia upatanisho hata kati ya watu waliotofautiana sana
(Waef 2:11-22): 11 Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya
mwili, mnaoitwa “Wasiotahiriwa” na wale wanaoitwa “Waliotahiriwa,” yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika
kwa mikono—12 kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa
maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani. 13 Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi
mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. 14 Kwa maana yeye ndiye amani yetu,
aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga, 15 Naye
akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili
kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani, 16 Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika
mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba. 17 “Akaja akahubiri amani
kwenu ninyi mliokuwa mbali, na amani kwao wale waliokuwa karibu”; 18 Kwa maana kwa yeye sisi sote
tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja. 19 Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali
ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu, 20 Mmejengwa juu ya msingi wa
mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. 21 Katika yeye jengo lote
linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana, 22 Katika yeye ninyi nanyi
23
Kwa kuwa msamaha ni jambo la katikati kwa Ukristo, kanisa linatakiwa kuona sehemu ya wajibu wake katika kusaidia
na kuwezesha mchakato wa msamaha na upatanisho. Kwa hakika, utafiti unaonyesha kwamba “watu wanaopta msaada
kutoka marafiki katika makundi ya kanisani husamehe zaidi kuliko watu wa kanisani ambao hawajihusishi na vikundi”
(Worthington, 2003: 70).
24
Jina lililotafsiriwa“upatanisho” ni katallagē, ambalo lina maana ya “mabadiliko au kupatanishwa kutoka kwenye hali ya
uadui kati ya watu na kuwa katika hali ya urafiki” (Zodhiates, 1993: katallagē; tazama pia Danker, 2000: katallagē,
“kuanzisha upya kwa uhusiano ulioingiliwa au kuvunjika”). Neno liliotafsiriwa “kupatanishwa” ni lile lile katallassō,
ambalo lina maana ya “kubadilika kwa ukatili kuwa uhusiano wa kirafiki, patanisha” (Ibid.: katallassō).
26
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho. (Tazama pia Warumi 10:12; 1 Wakor 12:13;
Wagal 3:28; Wakol 3:11)
A. Mgawanyiko mkubwa kati ya watu katika Agano la Kale, na moja pekee wenye umuhimu wa kitheolojia,
ni mgawanyiko kati ya Waisraeli na Mataifa; katika Kristo mgawanyiko huo haupo tena; kwa hiyo, watu
wote ni sawa mbele za Mungu
Kwa sababu uadui mkubwa na ukuta mkubwa unaotenga kati ya watu umeshaondolewa na Kristo,
uadui mdogo na kuta zinazotugawa vile vile zimeondolewa; matokeo yake, katika Kristo hakuna vikwazo vya
upatanisho kati ya makundi yoyote au watu.
B.Kusudi la Kristo ni kwamba sisi sote tuwe “mtu mpya” na tuwe na amani; kwa hiyo, kuishi kwetu kama
wamoja na wenye amani kila mmoja kwa mwenzake ni “ishara ya nje inayoonekana”kwamba sisi kwa
hakika tupo ndani ya Kristo.
C. Kile alichofanya Mungu kwa ajili yetu (iliyoelezwa kwenye kifungu hapo juu), inatakiwa ifanye
upatanisho kati yetu sisi na watu wengine kuwa kiini katika maisha yetu (kama Paulo alivyoeleza katika
Waefeso wengine wote)
Sande anafafanua jinsi gani mwitikio wetu kama wapatanishi na wafanya amani unavyotakiwa kutiririka
kutoka kwenye kupatanishwa kwetu na Mungu kwa njia ya Kristo: “Barua ya Paulo kwa Waefeso kimsisitizo
ililenga juu kufanya amani. Sura tatu za kwanza zinatoa maelezo matukufu ya mpango wa wokovu wa Mungu.
Katika sura ya nne, Paulo anaanza kuelezea jinsi tutakavyoitikia kwa kile Kristo alichofanya kwa ajili yetu.
Tazama kwa makini kile alichoweka Paulo katika mwanzo wa orodha yake ya matumizi ya Injili kwa vitendo:
‘Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa;
kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; na kujitahidi kuuhifadhi umoja
wa Roho katika kifungo cha amani (Waef 4:1-3). Neno la Kigiriki linatafsiriwa ‘fanya kila juhudi’ katika fungu
hiki ina maana ya kujitahidi kwa nguvu, kwa makini, na kwa uangalifu. Ni neno ambalo amelitumia mkufunzi
wa wapiganaji wakati alipotuma watu kupigana hadi kifo kwenye Coliseum: ‘Fanya kila juhudi kubaki hai leo!
Kwa hiyo pia mkristo anatakiwa kulilia amani na umoja. Bila shaka, bidii ya mdomoni na kujitahidi kwa juu juu
katika upatanisho inaangukia chini sana ya kile Paulo alichokuwa nacho katika ufahamu wake.” (Sande, 2004:
52)
III. Kupatanishwa kwetu mmoja kwa mwingine ni muhimu kiroho na kunahusiana na kumwabudu
kwetu Mungu (Mathayo 5:21-26): 21 “Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, ‘Usiue,’ na mtu akiua,
itampasa hukumu.’ 22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu
‘akimfyolea ndugu yake,’ itampasa baraza; na mtu ‘akimwapiza,’ itampasa jehanum ya moto. 23 Basi ukileta
sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, 24 iache sadaka yako
mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako. 25 Patana na
mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi
akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani. 26 Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti
ya mwisho.”25
A. Katika kifungu Yesu anaweka wazi mwunganiko uliopo kati ya sisi kupatanishwa na watu wengine na
kupatanishwa kwetu na Mungu.
B. Kifungu kinadhihirisha umuhimu ambao Mungu ameuweka kwenye upatanisho kati ya watu-ni kuakisi
“moyo wa ufalme”
Dallas Willard anafafanua jinsi ilivyo ya ajabu kanuni ya Math 5:23-24 kwa namna hii: “Wewe upo na
wasimamizi wa hekalu mbele ya madhabahu, na tayari unataka kutoa sadaka kwa Mungu. Ni moja ya tendo la
kiibada lililo takatifu sana katika maisha ya mtu mwaminifu. Uzoefu ni kwamba hili halitakiwi liingiliwe na
lingine lolote isipokuwa baadhi ya mambo mengine muhimu zaidi ya kiibada yanayohitaji mwitikio wa haraka.
Ghafla, katikati kabisa ya yote hayo, unamkumbuka ndugu ambaye anakukasirikia. Ukitambua
umuhimu wa hiyo nafsi kupata pumziko, na kuumizwa kutokana na tofauti iliyopo kati yako na yeye, unaacha
hilo tendo. Unatoka na kumtafuta ili kupatana naye. Hiyo inafafanua uzuri chanya wa moyo wa kifalme.
25
Neno liliotafsiriwa“kupatanishwa” katika 5:24 ni diallassomai. Ni sawa na maana ya katallassō, hiyo ni., “kurejeshwa
kwenye hali ya kawaida kimahusiano au kuwa na amani na mtu fuulani, kupatanishwa” (Danker 2000: diallassomai).
27
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
Kupata matokeo kamilifu tunatakiwa kujiona wenyewe kana kwamba tunaolewa/tunaoa au tunabatizwa
au tunawekwa wakfu kwa kazi fulani maalumu, kama vile mchungaji. Katika mchakato huo, tunatoka nje
kutafuta upatanisho na mtu ambaye hata hayupo hapo. Hiyo ni picha ya upendo wa kifalme ambao ndiyo haki
ya kifalme.” (Willard 1997: 156)
IV. Wakristo wameagizwa na Kristo na mitume wafanye kila wawezalo kuishi kwa amani wao kwa
wao na pamoja na watu wote.
A. Kristo alituamuru sisi kuwa na amani kila mmoja na mwenzake (Marko 9:50): Chumvi ni njema; lakini
chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee? Mwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa
ninyi.
B. “Kila waraka katika Agano Jipya una amri ya kuishi kwa amani kila mmoja na mwenzake” (Sande 2004:
51).
1. Warumi 12:18: Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. (Tazama pia 2
Wakor 13:11; 1 Wathes 5:13)
2. Warumi 15:5-7: 5 Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa
mfano wa Kristo Yesu; 6 ili kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa
Bwana wetu Yesu Kristo. 7 Kwa hiyo mkaribishane ninyi kwa ninyi, kama naye Kristo
alivyotukaribisha, ili Mungu atukuzwe.
3. 1 Wakor 1:10: Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene
mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.
4. Wakol 3:15: Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena
iweni watu wa shukrani.
V. Kristo na Mitume walidhihirisha upatanisho kwa vitendo kwa maisha yao wenyewe.
A. Kristo alidhihirisha upatanisho katika maisha ya hapa duniani. (Warumi 5:8-11): 8 Bali Mungu aonyesha
pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye
dhambi. 9 Basi zaidisana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.
10
Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya
kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake. 11 Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa
Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeyesasa tumeupokea huo upatanisho.
B. Kristo anaendelea kudhihirisha upatanisho katika jukumu lake kama kuhani mkuu (Waeb 7:23-25):
23
Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu wazuiliwa na mauti wasikae; 24 bali yeye, kwa kuwa
akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. 25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao
Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee. (tazama pia Warumi 8:34; 1 Yoh 2:1)
C. Mitume walidhihirisha upatanisho katika maisha yao: linganisha Math 20:20-24 na Matendo 1:13-14;
Matendo 15:36-40 with 2 Tim 4:11; tazama pia Filemoni 10-18.
VI. “Tunaposhindwa kutatua mgogoro sisi wenyewe, Mungu analiagiza kanisa liingilie na kuleta
hekima, rasilimali na mamlaka yake ili kushughulikia tatizo (Math 18:16-17; Filemoni 4:2-3; 1 Wakor
6:1-8)” (Sande 2004: 14).26
A. Kwa sababu kanisa ni mwili mmoja, wenye “viungo” vingi tofauti vyenye vipawa mbalimbali, ni muhimu
kutambua na kuwafunza watu wanaoheshimika, wenye hekima, wenye ukomavu, wanume na wanawake wa
kimungu katika kanisa wanaoweza kutumika kama washauri, wapatanishi, au wasuluhishi kuwezesha kati
ya ndugu wengine kanisani (na kati ya wasio washirika wa kanisa pia).
26
Nyongeza F kwa mujibu wa Sande mpatanishi ni mtu anaye “tengeneza utamaduni wa amani katika kanisa lako.” Taasisi
yake, Huduma ya Upatanisho, ina maelekezo kuhusu mafunzo kwa ajili ya mpatanishi, kielimu, na shughuli za kipatanishi.
Mawasiliano kwa ajili ya Huduma ya Upatanisho ni kama ifuatayo: anwani—P.O. Box 81130, Billings, MT 59108, U.S.A.;
simu—(406) 256-1583; barua pepe—[email protected]; tovuti—www.HisPeace.org.
28
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
B. “Wapatanishi wanaweza kufanya majukumu mbalimabali katika mgogoro” (Sande 2004: 191).
Sande anaeleza kwamba majukumu hayo ni: 1. Kuwasaidia watu walio na mgogoro kufanya uamuzi
unaohitajika ili kurejesha amani; 2. Kuwezesha mawasiliano kwa kuutia moyo kila upande kumsikiliza kila
mmoja wao kwa makini; 3. Kusaidia kutambua ukweli kwa kusikilizana kwa makini wao kwa wao, kwa kuuliza
maswali yanayofaa, na kwa kuwasaidia watu walio na mgogoro kupata ukweli zaidi; 4. Kutoa ushauri wa namna
ya kushughulika na tatizo (kama ilivyoelezwa katika Matthayo 18:17 na 1 Wakorintho 6:1-8); 5. Kuhimiza toba
na kukiri kwa upande mmoja au kwa wote kwa kuonyesha tabia yoyote ambayo haiendi sawa na mafundisho ya
Biblia; 6. Kuwezesha usuluhishi wa kibiblia kwa mambo yahusuyo vitu kwa kuelekeza pande hizo zilizo na
mgogoro kufuata kanuni bora na mifano ya Maandiko; 7. Kushauri suluhu za vitendo kwa matatizo maalumu
kutokana na ufahamu wao wenyewe na uzoefu wao (Ibid.).
A. Msamaha ni mwitikio wa mtu mmoja wa kimaadili kwa kosa la mtu mwingine; upatanisho ni kuja kwa
watu wawili pamoja ili kurejesha uhusiano ambao umevunjika kwa kukosa uaminifu (i.e., kuondoa kikwazo
cha kimaadili kwenye ushirika)
“Inahitaji mtu mmoja kusamehe. Wanahitajika watu wawili kupatana tena.
Msamaha hutokea ndani ya mtu aliyejeruhiwa. Kupatana tena kunatokea kati ya watu.
Tunaweza kumsamehe ambaye kamwe hajasema samahani. Hatuwezi kupatana tena kikamilifu kama asipokuwa
ametubu kikamilifu.
Tunaweza kusamehe hata kama hatumwamini mtu aliyetukosea mara moja na bila kutukosea tena. Kupatana
kunaweza tu kutokea kama tunaweza kumwamini mtu aliyetukosea mara moja na kwamba hawezi kutukosea
tena. Msamaha hauna kamba zilizofungamanishwa. Upatanisho una kamba zilizofungamano nao.” (Smedes
1996: 27)
A. Upatanisho ni ushahidi wa nguvu za Mungu, na unadhihirisha utii wetu kwa amri ya muhimu sana
ambayo Kristo ametupa usiku kabla ya kusulubiwa kwake
1. Katika usiku wake wa mwisho kabla ya kusulubiwa, Yesu alisema hivi: Amri mpya nawapa,
Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote
watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. (Yoh 13:34-
35)
2. Bila ya upatanisho tutashindwa kuuonyesha ulimwengu uthibitisha mmoja muhimu sana wa sisi
kwamba ni wanafunzi wa Kristo.
27
Sehemu hii kimsingi ni kutokana na Worthington 2003: sura ya 9-12; Jeffress 2000: sura ya 5; na Smedes 1996: sura ya 3;
na kiwango cha juu zaidi na Enright 2001: sura ya 15.
28
Chati ya ulinganisho inatokana na Worthington 2003: 171, Jedwali namba 9.1.
29
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
C. Kuishi kwetu kwa maelewano na, kwa baraka, na wengine matokeo yake ni Mungu kutubariki sisi
(1 Pet 3:8-9): 8 Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu,
wasikitikivu, wanyenyekevu; 9 watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa
sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.29
1. Amua. Kwanza hutangulia uamuzi, kwamba tunahitaji kupatana au la. Upatanisho huhitaji kwenda
pande zote mbili, kwa hiyo pande hizo zinaweza kukwamisha katika hatua yoyote. Upatanisho unahitaji
29
“Baraka” tunazoweza kupokea kutoka kwa Mungu zinahusiana na “tabia ya haki ambayo inaamriwa na Petro kwa
[waaminio] inaonekana katika mstari wa 8-9a” (Grudem 1988: 147). Ingawa baadhi ya waliotoa maoni yao wanakoleza
“baraka” wakimaanisha wokovu wa mtu wa siku ya mwisho, wazo lenye nguvu pia linaweza kutolewa kwamba kile
alichomaanisha Petro ni kwamba kuishi maisha ya maelewano na kuwabariki wengine kama malipo kwa mabaya kunaleta
baraka kutoka kwa Mungu katika maisha ya sasa (cp., Michaels 1988: 178-79, pamoja na Grudem 1988: 148-49).
30
Sande ana mtindo wa mchakato wa urejesho wa aina hiyo wenye hatua nne:: (1) toba; (2) kujipima mwenyewe; (3)
kuungama; na (4) badiliko la kibinafsi (Sande 2004: 118-35).
30
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
muda, juhudi, unyenyekevu, na hatari ya kuumizwa tena au kutumiwa kwa maslahi binafsi na mtu
mwingine.
a. Mtu anaweza asitake kupatana ikiwa: (1) anapenda kuwa mbali na haoni sababu ya kuanza
upya mahusiano; (2) una hatarisha afya au si salama kufanya hivyo (kuna hatari ya kuumizwa
kimwili au maumivu mengine); (3) mmoja amekuwa akikosa uaminifu mara kwa mara na
huonyesha toba au majuto kidogo au haonyeshi kabisa; (4) maumivu na jeraha, sasa kwa
kiwango cha chini, ni makubwa sana; (5) mmoja amekufa, hayupo, au kwa sababu nyingine
haiwezekani kupatana.
b. Watu huamua kupatana kwa sababu: (1) hawahitaji kukubali kushindwa katika mahusiano;
(2)wanathaminiana kila mmoja na mwenzake na katika mahusiano; (4) hawako tayari kurudi
kwenye hadhi yao ya kawaida lakini wanataka mahusiano imara na yaliyo bora zaidi; (5)
wanaamini kwamba kupata upatanisho ni dhahiri kutakuwa na matokeo chanya zaidi kuliko
kutofanya chochote.
c. Ni lazima tuamue jinsi ya kupatana. Upatanisho hutokea kwa njia mbili:
(1) Upatanisho mara nyingi huja kikamilifu, bila ya pande husika kujadiliana kwa wazi.
Upatanisho usio wazi unahusisha: kuacha ukali; kuja pamoja (nayo ni, kwa ajili ya
jukumu la pamoja); kuungana pamoja na (au kuunganishwa pamoja na) mtu wa tatu
kwa ajili ya shughuli mbalimbali; kuwa na mtazamo chanya na kukamilishana mmoja
kwa mwingine; tukitambua umoja wetu na Kristo, ambayo inaweza kusaidia kuvunja
“kuta za mgawanyiko” za ufahamu na za kihisia” (Waef 2:14-16).
(2) Upatanisho ulio wazi unatokea wakati pande husika zinapokuja pamoja
kushughulikia kipekee tatizo na kurejesha uhusiano uliovunjika.
(A) Ingawa baadhi ya watu hufikiri kwamba Math 18:15-20 ni aina fulani ya
“sheria” inayolazimisha kuwa na mazungumzo binafsi na ya siri na mtu
aliyetukosea kabla ya kuwaomba wengine kujihusisha na hali hiyo, sivyo ilivyo.
Yakobo (Mwanzo 32-33), Abigaili (1 Samweli 25:18-35), Ayubu (2 Samweli
14:1-23), na Barnaba (Matendo 9:26-27) wote walihusika kwa niaba ya
wengine, au waliwaomba wengine kujihusisha, ili kuleta upatanisho kabla ya
pande husika zilizo na uhusiano uliovunjika kukutana peke yao.
(B) Katika kujua jinsi ya kuanza mchakato wa upatanisho ulio wazi:
“Mazungumzo binafsi mara zote ni mazuri zaidi, lakini kwa visa baadhi
kuhusisha watu wengine moja kwa moja itakuwa ni vizuri zaidi. Kuna hali
kadhaa ambazo zinaweza kudhihirisha ukweli huo leo:
Wakati unahusika na mtu anayetoka kwenye utamaduni au desturi
ambayo ni kawaida kutatua matatizo kupitia watu wa katikati kama vile
wawakilishi wa familia au viongozi wanaoamiwa
Wakati unaenda kwa mtu fulani wewe mwenyewe na kibinafsi ni wazi
kwamba hawataweza kuonekana machoni kwa wengine;
Wakati pande husika wanaweza kuhisi kuogopeshwa na mtu mwingine,
labda kwa sababu ya ujuzi wa kuzungumza au nafasi katika mamlaka au
ushawishi;
Wakati mtu mmoja amenyanyaswa na mwingine na kuna uwezekano
kwamba mnyanyasaji atatumia mazungumzo ya siri kumrubuni au
kumnyamazisha mtu aliyenyanyaswa;
Wakati upande wa tatu alio na uhusiano wa karibu kuliko wewe ulivyo
na mtu anayeweza kukutwa na dhambi, na huo upande wa tatu upo tayari
kuibua jambo pamoja na mkosaji.” (Sande, 2004: 146-47)
d. Ni lazima kuamua ni wakati gani tupatane. Msamaha wa Maamuzi na Kihisia unaweza
kufanyika kwa haraka wakati mwingine; upatanisho karibu mara zote huhitaji kipindi cha muda.
Wakristo wanatakiwa kutafuta fursa za kuanzisha mchakato wa upatanisho. Kabla ya kuanzisha
upatanisho ulio wazi, tunapaswa kutathmini nia zetu wenyewe na hali za ufahamu na hisia (je
sisi tuna msongo sana? Tuna hasira?—bila shaka ni muhimu kuomba na kushughulika na hayo
kwanza). Tunahitajika kumtathmini mtu mwingine na mazingira, na kuomba kwa ajili ya
uongozi wa Mungu. Pamoja na hayo tunapaswa siku zote kutenda kwa namna inayoendana (na
inayowezesha) upatanisho usio wa wazi.
2. Jadiliana. Mara uamuzi unapofikiwa, pande zinazohusika zinahitajika kuja pamoja na kujadili
uhusiano wao, mgawanyiko ukiotokea kati yao, na jinsi ya kurejesha urafiki au uhusiano mzuri.
31
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
32
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
NUKUU ZILIZOTUMIKA
Aland, Barbara, Kurt Aland, Johannes Karavidopoulos, Carlo Martini, and Bruce Metzger, eds. 2001. The Greek New
Testament, 4th rev. ed. Stuttgart: Deutsche Bibelgesellschaft.
Chapman, Gary, and Jennifer Thomas. 2006. The Five Languages of Apology. Detroit: Thorndike.
31
Mwendelezo huu unaendana na mtazamo wa Sande kwamba mzizi wa mgogoro ni “matakwa yasiyofikiwa katika mioyo
yetu,” ambazo pia zinafuata mchakato wa hatua nne: (1) Ninatamani—mgogoro huanza na aina fulani ya tamaa (ambayo,
yenyewe, inaweza kuwa na maana au haina maana; (2) Ninahitaji—tama isiyofikiwa inakuzwa, na inageuka kuwa hitaji
“ambalo ni lazima lifikiwe ili kuridhika na kutosheka,” na inaweza kuelekea kwenye uchungu, kinyongo, na kujihurumia
linazidi kutokufikiwa; (3) Ninahukumu—wakati wengine wanashindwa kutimiza tamaa yetu na kuishi kulingana na
matarajio yetu, tunawakosoa na kuwahukumu wao katika mioyo yetu kama siyo kwa maneno yetu; (4) Ninaadhibu—
mtazamo wa kuhukumu hutupeleka kwenye mtazamo wa kuhukumu unaotuongoza kwenye hisia za kutafuta jinsi ya wazi
au isiyo wazi ya kuwadhibu watu na kuwalazimisha kufanya matakwa yetu . (Sande, 2004: 102-09)
33
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
Danker, Frederick W., ed. 2000. A Greek-English Lexicon of the New Testament and Other Early Christian Literature, 3d
ed. Chicago: University of Chicago Press.
Ellingworth, Paul. 1992. “Forgiveness of Sins.” In Dictionary of Jesus and the Gospels, ed. Joel Green, Scot McKnight,
and I. Howard Marshall, 241-43. Downers Grove, IL: InterVarsity.
Enright, Robert. 2001. Forgiveness Is A Choice. Washington, DC: American Psychological Association.
Grudem, Wayne. 1988. The First Epistle of Peter (TNTC). Grand Rapids, MI: Eerdmans.
Jeffress, Robert. 2000. When Forgiveness Doesn’t Make Sense. Colorado Springs, CO: Waterbrook.
Klassen, Daniel. n.d. The Forgiveness Workbook. Thunder Bay, Ontario, Canada: Lakehead University.
McCullough, Michael. 2000. “Forgiveness as Human Strength: Theory, Measurement, and Links to Well-Being.” Journal
of Social and Clinical Psychology 19, no. 1: 43-55.
Sande, Ken. 2004. The Peacemaker, 3rd ed. Grand Rapids, MI: BakerBooks.
Smedes, Lewis. 1984. Forgive and Forget: Healing the Hurts We Don’t Deserve. San Francisco: Harper & Row.
Solzhenitsyn, Aleksandr. 1985. The Gulag Archipelago 1918-1956. Translated by Thomas Whitney and Harry Willetts.
Abridged by Edward Ericson, Jr. New York: Harper & Row.
Witvliet, Charlotte vanOyen, Thomas E. Ludwig, and Kelly L. Vander Laan. 2001. “Granting Forgiveness or Harboring
Grudges: Implications for Emotion, Psychology, and Health.” Psychological Science 12, no. 2: 117-23.
Zodhiates, Spiros, ed. 1993. The Complete Word Study Dictionary: New Testament, rev. ed. Chattanooga, TN: AMG.
NYONGEZA
Mfano wa Msamaha wenye msingi wa maamuzi kwa ajili ya urejesho wa Ndoa na Mahusiano ya
Kifamilia32
Mfano huu umeandaliwa kwa ajili ya wanandoa wakristo. Hata hivyo, unaweza kutumiwa na wakristo
wanaokutana na matatizo katika mahusiano ya aina nyingine. Unaweza ukawa na msaada pia kwa wasio
wakristo, lakini siyo sana kwa sababu kanuni zake ni za kibiblia ambazo zinaweza zisikubalike kwa wale wasio
wakristo.
Kikao cha msamaha kinachohusisha mshauri nasaha na wanandoa kwa kawaida ni kirefu (angalau saa
tatu kwa kiwango cha chini) na kina hatua 13. Hizi hatua zimepangwa katika sehemu tatu: (1) kutoa maana na
maandalizi (Hatua ya 1-3), ambayo inahusisha mjadala kati ya mshauri nasaha na mwanandoa; (2) kutafuta na
32
Mtindo huu unatokana na rasimu za makala zifuatazo: Frederick A. DiBlasio, “Maandiko na Msamaha: Kujihusisha na
Wanandoa wa Kikristo na Familia,” Ndoa na Familia: Gazeti la Kikristo 2 (1999): 247-58, na Frederick DiBlasio na
Robert Cheong, “Upendo wa Kikristo na Msamaha katika Ushauri wa Ndoa: Nadharia na Vitendo” (Iliyotolewa ma na
waandishi kwa Ndoa na Familia:Gazeti la Kikristo, katika machapisho).
Kwa kuongezea, ECLEA katika tovuti yake inayo (www.eclea.net) yote mawili Maelekezo na Mwongozo wa
Kiongozi, na Maelekezo ya Mshiriki kwa ajili ya kozi ya kukuza msamaha ya Everett L. Worthington, Kupata Msamaha:
Masomo sita ya Kivitendo ya Kufanyika Mkristo mwenye kusamehe zaidi. Dr. Worthington ametoa ruhusa ya kupakua
mafunzo haya, kuchapishwa, na kutumiwa bila malipo.
34
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
kutoa msamaha (Hatua ya 4-12)—baada ya mwanandoa mmoja kumaliza hatua zote kati ya hatua ya 4-12
mwanandoa mwingine huanza; na (3) kikao huisha kwa tendo la maadhimisho ya kiibada (Hatua ya 13).
Mwanandoa bila shaka atahitaji kupata ushauri nasahau siku zijazo baada ya kikao cha msamaha, lakini
umalizaji wa mafanikio wa kikao kirefu cha msamaha kinatakiwa kupunguza idadi ya vikao vingine vya ushauri
nasaha.
Hatua ya 1: Maana ya msamaha hujadiliwa. Mshauri nasaha anapata ruhusa ya kuongea kuhusu maana
ya msamaha, kutoka kwa washauriwa kwa kuwa ni kiini cha imani. Wote waongee kuhusu maana ya msamaha.
Mshauri nasaha hujadili nini Biblia inasema kuhusu msamaha na upendo. Mshauri nasaha atajikita kwenye
utaratibu unaotegemea maamuzi. Mshauriwa ni lazima akubali kuwa uamuzi wa kusamehe hauhusishi ufahamu
wa kuachilia na hitaji la kutolipa kisasi, bali pia unahusisha matendo ya msamaha ya kujikana mwenyewe na
kupenda kama Kristo alivyofanya. Kuwaelekeza mwanandoa kwenye maandiko ni muhimu, kwa kuwa wakristo
wengi wanataka mawazo yao, maneno na matendo yaende sawasawa na Maandiko.
Hatua ya 2: Nia ya kila mtu kuwa na fursa ya kutafuta msamaha kwa ajili ya matendo yake yasiyo
sahihi hujengwa. Wenzi huwa na fursa ya kuungama makosa yao kila mmoja kwa mwenzake mbele ya
mshauri. Nia siyo kutetea matendo yao, au kuwashambulia wenzi wao kwa makosa yao, lakini kujielekeza
kwenye madhaifu yao wenyewe na kutubu kwa ajili ya makosa yao. Mshauri anaweza akasema kitu kama:
“Tunahitaji kuweka mwongozo kwa ajili ya kikao chetu. Wenzi mara nyingi huja na mambo mengi kwenye
ushauri kuhusu tabia inayoumiza ya mwingine, lakini mara chache hujikita kwenye makosa yao wenyewe bila
kusukumwa. Ukikubali kuendelea na kikao, upo tayari kujikita katika mchango wako mwenyewe kwenye tatizo
ukifika wakati wako kufuata zile hatua na kuachana na matarajio ya yale ambayo mwenzako itampasa
kuyaungama? Kama mwenzako hataibua jambo ambalo ni muhimu kwako, tutalishughulikia katika kikao
kijacho”
Hatua ya 3: Utangulizi kuhusu tiba ya msamaha na uamuzi ya kwamba inaendelea au la. Kwa kawaida
inafaa sana kuanza na mwanandoa ambaye ametenda kosa baya zaidi. Kila mwanandoa ni lazima aweke
maamuzi katika mambo machache ambayo kwayo wanataka kusamehewa. Mshauri atatambua kama wana
maudhui yanayofanana. Mshauri anaweza kusema: “Kikao cha Msamaha uliopangiliwa hakifuati kila kitu
kuhusu ushauri nasaha. Ukimkubalia mwanandoa kuendelea [Mwanandoa A] atafuata hatua kuanzia ya 4-12
katika mtiririko, na kisha atampa nafasi [Mwanandoa B] aendelee (mshauri nasaha anaweza akachapa na
kukabidhi nakala ya hatua kwa muhutasari na kwa ufupi). Nitahusika kikamilifu katika kikao, kutunza kikao
kifuate mwelekeo sahihi na kwa msaada wako, na kufanya maamuzi, kwamba ni maelezo yapi ni ya kufaa
katika kikao cha msamaha na nini kiwekwe kama kumbukumbu kwa wakati unaofuata.”
Hatua ya 4: Tamko lenye makosa. Mwanandoa ni lazima aeleze kwa wazi tabia yao inayoumiza.
Inahitaji kuelezwa kwa namna ambayo inaonyesha ufahamu kuwa lilikuwa ni kosa, linaumiza na kwamba
haikuwa haki. Mara nyingi mwanandoa anaweza akahusisha katika tamko lake kitu fulani kuhusu matendo ya
mwanandoa mwenzake. (k.m., mwanaume hutafuta msamaha kwa maneno akimkosoa mke wake kwenye
hadhara kwa sababu asili yake ya makosa na isiyovumilia). Akihusisha mtazamo wake juu ya matendo ya mke
wake hupunguza uwezo wake na kuongeza utetezi kwa upande wa mke wake. Mshauri kwa hiyo ni lazima
amsaidie mwanandoa kuhusisha sehemu yake tu ya tatizo. Inasaidia kumwuliza mwanandoa, Je kosa hili
lilikuwa baya?” Kama mwanandoa akisita, mshauri anapaswa kuibua hilo na kumfanya mwanadoa au kulikubali
hilo kosa na kuonyesha kuwa anaamini ni baya, au kulifikiria tena. Katika visa vingi, maelezo ya kosa yanaweza
kuibua mengine yaliyokuwepo.
Hatua ya 5: Mkosaji anatoa maelezo. Mshauri anaanza hatua hii kwa kuruhusiwa na mtu aliyekosewa
kujaribu kujua sababu za kosa la mwenzi wake (kupata ruhusa kunamhusisha mwenzi aliyekosewa kama
muhusika aliye macho kutambua tabia iliyosababisha maumivu). Mshauri anaweza akaeleza wazi kwamba
baadhi ya makosa kwenye ndoa yana maelezo, lakini maelezo hayo wakati mwingine yanapotezwa kwa sababu
ya majeraha au maumivu yaliyopatikana kwa pande zote mbili. Mshauri atoe tahadhari kwamba maelezo hayo
yasiwe kama “utetezi” lakini ni sehemu ya kutafuta habari itakayotuwezesha sisi kufanya tathmini ya kina ya
kosa. Kutafuta sababu zilizosababisha kosa inaweza kutufikisha kwenye kutambua hali tabia zilizokuwepo kabla
ya kuoana. Hili, hatimaye, inaweza kusababisha wanandoa, kuwa na ufahamu mkubwa, na kuhurumiana, kila
mmoja wao.
Hatua ya 6: Maswali na majibu juu ya kosa. Wanandoa wanatakiwa kujitahidi kufahamiana wao kwa
35
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
wao. Hata hivyo, maswali mengi wanayouliza yanatumika “kutafuta kueleweka” kuliko kutafuta kuelewa na
kuibua taarifa. Mshauri anaweza kusema: “Kama inavyoonekana kuwa jambo la kustaabisha, mara chache
wanandoa hupata majibu sahihi kwa maswali yao kwa sababu ya uwepo wa mazingira ya kujitetea dhidi ya
kosa. Maswali huulizwa kwa ukali au huulizwa kwa namna ya kujitetea. Huu ni wakati wa kupata taarifa kutoka
katika roho ya upendo. Embu tufanye kazi kwa pamoja ili kuelewa kwa hakika tatizo hili kwa njia ya kuuliza
maswali. [Mwandoa B] una swali lolote kwa [mke/mume] wako?” Kutoa majibu na ukweli ni kumsafisha
mkosaji na kuleta wepesi katika kusamehe. Mshauri anaweza kuchukua nafasi yenye umuhimu mkubwa
kikamilifu katika kusaidia kuunda maswali na kuwaweka wanandoa katika mwelekeo sahihi.
Hatua ya 7: Mtu aliyekosewa hutoa mwitikio wa kihisia. Ukaribu unaweza kuja tu ikiwa mwanandoa
ataweza kuungana katika hatua ya hisia. Mtu aliyekosewa anataka mkosaji asikie na kuelewa maumivu na hisia
lakini anaweza kuwa na ugumu katika kuelezea hisia zake. Hapo tena, msahauri anatakiwa ahusike katika
umuhimu mkubwa kusababisha nia isi-yojitetea. Mshauri anaweza kusema: “Ingawa inaweza kuwa ni muhimu
kwa ajili ya [Mwanandoa B] kueleza maumivu yake inaweza kuwa vigumu kwa sababu anaogopa kuumiza
moyo wako, je wewe [Mwanandoa A] utampa ruhusa aeleze moyo wake kikamilifu kwako kuhusu maumivu
yake?” (Mwanadoa anapotoa ruhusa kwa mwingine kuelezea hisia zake, wanahama kutoka kwenye hali
kujitetea binafsi na kuwa katika hali ya kupokea.) Mwanandoa aliyekosewa anaweza kueleza alivyoumia kwa
wakati ule na jinsi anavyojisikia sasa baada ya kujifunza katika kipindi cha ushauri.
Hatua ya 8: Mkosaji anaonyesha huruma na majuto kwa ajili maumivu aliyosababisha kwa mwenzake.
Mkosaji kueleza ipasavyo maumivu na huzuni hutoa utambuzi kwamba mateso ya mwanandoa yameeleweka na
kutambuliwa. Hili, hatimaye, inatufikisha kwenye huruma na husaidia katika kuleta msamaha wa kihisia.
Wanandoa wengi wanaweza kuwa wabinafsi sana na kuwa vigumu kuhisi au kuelezea huruma zao kwa
mwingine. Mshauri anaweza akasaidia kwa kuuliza swali kama, “Wakati mke wako aliposema ameumia sana
kwamba aliamka akilia usiku, unapofikiri hilo unapata hisia kama ipi?” Mshauri anaweza kumwomba kila
mwanandoa aseme kwa muhutasari majuto na huruma iliyoelezwa na mwenzake.
Hatua ya 9: Mkosaji anaandaa mpango kukomesha/kuzuia tabia. Ili mtu atafute msamaha katika kweli
ina maana kwamba mkosaji anapanga kukomesha tabia inayosababisha kosa na kuzuia isitokee tena siku za
mbeleni. Msamaha unawezeshwa pale ambapo tendo la kurekebisha limepangwa na mfumo wa uwajibikaji
umewekwa. Mpango unahitaji kuwa mahususi na uwe umewekwa na mkosaji kwa msaada wa mwenzi wake na
mshauri. Mshauri anaweza kumwomba Roho Mtakatifu kuleta mawazo kwenye ufahamu na anaweza kusema:
“Kwa nini tusianze na mambo ambayo unataka kujitoa kuyafanya, na labda unaandaa mawazo ambayo
yatakuhakikishia kuona kwamba unajitoa kuyaishi hayo?” Mshauri anaandaa kumbukumbu ya maandishi ya kila
upande wa mpango na kuhimiza umuhimu wa wanandoa kutunza mpango ulioandikwa mahali panapofikika na
salama.
Hatua ya 10: Mwanandoa aliyekosewa ananyesha huruma kwa ajili ya moyo wa mkosaji ulioumia.
Matatizo ya ndoa mara zote yanahusisha maumivu yanayoonekana kwa mkosaji na vile vile kwa aliyekosewa.
Tabia ya mkosaji inaweza kwa sehemu ikaelezwa na maumivu yaliyopita katika mahusiano na/au maumivu
yalijitokeza huko nyuma. Zaidi, mkosaji ni lazima sasa ashughulike pia na aibu na hatia ya kumsababishia
maumivu kwa mwenzi wake. Mshauri anaweza kusema kwa mwenzi aliyekosewa: “Nimetambua kosa la mke
wako limesababisha maumivu makubwa kwako, lakini sasa tunaona hata yeye anaumia. Unaweza kuweka
katika maneno maumivu anayopitia?” Kama katika hatua ya 8, mshauri anaweza akasaidia mwenzi kupata
ufahamu wa huruma.
Hatua ya 11: Msisitizo kwenye uchaguzi na kujitoa kuachilia. Mshauri anawakumbusha wanandoa
mjadala wa hatua ya 1 kuhusu upendo na msamaha na kusamehe kwa kufanya maamuzi. Kama mwenzi
aliyekosewa akichagua kusamehe, yeye anajitoa kimakusudi kuachilia kosa na bila kulitumia kama silaha siku
za mbeleni. Hiyo haimaanishi kulazimika kuacha kuongelea tatizo; kwa hakika, kulifanyia kazi tatizo katika
ushauri kunaweza kuhitajika mjadala. Kwa hiyo ni lazima mjadala ufanyike kuhusu namna ya kuzuia kucheua
kosa na namna ya kushughulika na mawazo ya kulipiza kisasi ambayo yanaweza kujitokeza huko mbeleni
(tazama mjadala kuhusu kujitoa hadharani kusamehe na kushikilia msamaha katika sehemu ya V. “Msamaha na
Upatanisho,” hapo juu).
Hatua ya 12: Kuomba msamaha kirasmi. Ili msamaha uwe wazi, wenzi wanatakiwa watamke maneno
ombi na utoaji wa msamaha. Mshauri anaweza akasema: “Sasa ni wakati, kama [Mwenzi A] yupo tayari, kwa
ajili ya yeye kuomba msamaha mbele yangu kama shahidi. [Mwenzi B] kisha ataitika kama yeye atatoa
36
Hakimiliki © 2007-20147 na Jonathan Menn. Haki zote zimehifadhiwa.
msamaha au la.” Kuomba msamaha rasmi mbele ya shahidi inakazia kwamba uamuzi thabiti umefanyika kwa
ajili ya msamaha. Wanandoa wengi wanaweza kulia, kushikana mikono, au kupiga magoti kusisitiza toba yao na
majuto yao juu ya kosa. Baada ya msamaha kutolewa, mshauri anaandika tarehe kamili na muda na kuwaomba
wanandoa waandike mahali maalumu. Mshauri anaweza kusema: “Msamaha ulitafutwa na kutolewa mnamo saa
11:32AM katika tarehe hii. Tafadhali kumbuka zingatia kuweka kumbukumbu tarehe hii na muda kwa sababu ni
takatifu katika macho ya Mungu. Kama kuna maswali kuhusu uliomba au ulitoa msamaha, tafadhali kumbuka
muda na tarehe au jisikie huru kunipigia simu mimi kama shahidi.”
Hatua ya 13: Tendo la kusherehekea. Tendo la nje, la kusherehekea kati ya wanandoa litakazia
msamaha walioshiriki na husaidia kufanya maamuzi yao kuwa imara na ya kudumu kiufahamu, kihisia na
kiroho. Mshauri anaweza kuuliza: “Unawezaje kusherehekea msamaha uliotokea hapa—jambo litakalowakilisha
msamaha kama ishara—jambo la kisherehe?” Wanandoa wanaweza kuandika makosa yao kwenye karatasi na
kuchoma hayo makaratasi, kupanda mti maalumu, kuandika na kupeana barua za mapenzi, kupeana zawadi, au
kufanya jambo lingine lolote litakaloweka alama kwenye msamaha wao na mwanzo wa maisha mapya pamoja.
Hatua hii nzima inaweza kuwa ya kiukombozi, inayobadilisha uzoefu wa maisha unaoathiri mtu binafsi,
unaoathiri mahusiano katika ndoa, na kuwaleta karibu pamoja katika kuongezeka kwa ukaribu wao kwa Kristo.
MWANDISHI Jonathan Menn anaishi Appleton, WI, USA. Alipata B.A. yake katika Sayansi ya Siasa kutoka Chuo
Kikuu cha Wisconsin-Madison, na kuibuka na daraja la juu la heshima, mwaka 1974, na kuingizwa
katika jamii inayoheshimika ya Phi Beta Kappa. Kisha akapokea J.D. kutoka Cornell Law School,
magna cum laude, mwaka 1977, na akawa miongoni mwa Jamii ya Sheria inayoeshimika ya Coif.
Alitumia miaka 28 inayofuata akijihusisha na shughuli za sheria, kama wakili wa sheria
anayejitegemea kule Chicago na baadaye kama mdau Kitengo cha sheria cha Menn Law Firm kule
Appleton, WI. Mwaka 1982 akaamini na kuwa mfuasi wa Yesu Kristo. Upendo wake unaokua katika
theolojia ulimfanya ahitimu shahada yake ya pili katika chuo cha Trinity Evangelical Divinity School
kule Deerfield, IL. Akahitimu shahada ya pili ya theolojia kutoka TEDS, summa cum laude, mnamo
Mei 2007. Kati ya 2007-2013 alikuwa Mkurugenzi wa Equipping Pastors International. Sasa Jonathan
ni Mkurugenzi wa Equipping Church Leaders-East Africa (ECLEA). Machapisho yake yaliyosheheni
ya masomo ya Biblia yanapatatikana kwenye www.eclea.net. Jonathan anaweza kuandikiwa au
kuwasilana naye kupitia barua pepe hii: [email protected].
37