Peter Ustinov
Sir Peter Alexander Ustinov (16 Aprili 1921 – 28 Machi 2004)[1] alikuwa muigizaji, mwandishi, na mwanaharakati wa ubinadamu wa Uingereza. Akiwa msimuliaji hadithi mashuhuri duniani (raconteur),[2] alikuwa mtu wa kudumu kwenye vipindi vya mahojiano vya televisheni na mihadhara kwa muda mrefu wa kazi yake. Ustinov alipokea tuzo nyingi ikiwa ni pamoja na Tuzo mbili za Academy (Oscar), Tuzo tatu za Primetime Emmy, Tuzo moja ya Golden Globe, tuzo ya Silver Bear, tuzo ya Laurel, tuzo ya Photoplay, na Tuzo moja ya Grammy, pamoja na kuteuliwa kuwania Tuzo tatu za BAFTA, Tuzo mbili za Tony, Tuzo mbili za Laurence Olivier, na Tuzo moja ya Gemini. Mnamo mwaka 1992, Ustinov alitunukiwa Tuzo ya British Academy Britannia.[3]
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Peter Alexander Freiherr von Ustinov alizaliwa mnamo Aprili 16, 1921, katika mtaa wa 45 Belsize Park, London. Baba yake, Jona Freiherr von Ustinov, alikuwa na asili mchanganyiko ya Kirusi, Kijerumani, Kipolandi, Kiethiopia, na Kiyahudi.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.ebsco.com/research-starters/biography/peter-ustinov/
- ↑ https://www.britannica.com/biography/Peter-Ustinov
- ↑ https://travsd.wordpress.com/2021/04/16/peter-ustinov-turns-100/
- ↑ https://verbierfestival.com/en/musician/ustinov-peter/
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Peter Ustinov kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |