Nenda kwa yaliyomo

Keith Sweat

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Keith Sweat
Sweat mnamo mwaka 2023
Taarifa za awali
Amezaliwa22 Julai 1961 (1961-07-22) (umri 65)
New York City, Marekani
Aina ya muziki
Kazi yake
Miaka ya kazi1975–sasa
Studio
Ameshirikiana naLSG

Keith Sweat (amezaliwa Julai 22, 1961) ni mwimbaji, mtayarishaji, na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Marekani. Akiwa mmoja wa waasisi wa mtindo wa muziki wa new jack swing, anajulikana kwa rundo la nyimbo zake kali zilizovuma ikiwemo "I Want Her," "Make It Last Forever," "I'll Give All My Love to You," "Make You Sweat," "Get Up on It," "Twisted," na "Nobody." Ametoa jumla ya albamu 13 za kujitegemea — mbili zikiwa kama sehemu ya kundi la mastaa wa R&B LSG — na alianzisha makundi ya Silk na Kut Klose. Inasemekana kuwa muziki wa Sweat uliathiriwa na kiongozi wa bendi ya Slave, bwana Steve Arrington, pamoja na muziki wa Go-go.[1]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Keith Sweat alizaliwa mtaa wa Harlem, jijini New York, kwa mama yake Juanita Thompson, ambaye alikuwa msusi, na baba yake Charles Sweat, aliyekuwa mfanyakazi wa kiwandani.[2]: 206 [3] Baada ya kifo cha Charles Sweat mnamo 1973, Juanita aliwalea watoto wao watano peke yake.[4] Katika ujana wake, Sweat alitumbuiza kwenye ukumbi maarufu wa Apollo Theater, uliokuwa karibu na nyumbani kwao.[5]

Kabla ya kutoa albamu yake ya kwanza, Sweat alifanya kazi ya kupanga bidhaa usiku kwenye duka la Macy's, na baadaye akawa karani wa chumba cha barua kwenye kampuni ya udalali ya Paine Webber. Pamoja na kazi hizo, alipata shahada ya mawasiliano kutoka Chuo cha City College of New York.[6] “Nadhani kila mtu anapaswa kuwa na mpango mbadala. Kwa upande wangu, nilienda City College ya New York na kupata shahada yangu ya mawasiliano. Hivyo nilikuwa na 'mpango badala' ili nisipoteze fursa ya kuwa na maisha mazuri ya baadaye,” Sweat aliwahi kusema.[7]

Ndani ya miaka minne tu, alipanda vyeo na kufikia nafasi yenye mshahara mnono kama msaidizi wa udalali kwenye soko la hisa la New York (New York Stock Exchange).[8] Sweat pia alifanya kazi kama msimamizi katika soko la biashara la New York Mercantile Exchange.[4]

Kazi ya muziki

[hariri | hariri chanzo]

1975–1984: Mwanzo wa kazi na Jamilah

[hariri | hariri chanzo]

Sweat alianza safari yake ya muziki kama mwanachama wa bendi ya Harlem iitwayo Jamilah mnamo mwaka 1975.[9] Kupitia Jamilah, Sweat aliweza kukuza uwezo wake kama mwimbaji kiongozi kwa kutumbuiza katika maeneo ya New York, New Jersey, na Connecticut. Bendi hiyo ilianzishwa na mpiga besi Larry Peoples, mpiga gitaa Michael Samuels, na mpiga ngoma Walter Bradley.[10]

Baada ya kuondoka kwenye kundi hilo mwaka 1984 ili kuanza kazi ya peke yake, Sweat aliimba kwenye klabu za usiku mjini New York na kupata nafasi ya kurekodi na lebo huru ya Stadium Records. Alirekodi nyimbo mbili pekee akiwa Stadium, "Lucky Seven" na "My Mind Is Made Up." Hata hivyo, kwenye toleo la kwanza la Stadium, amewekwa kama mwandishi na mtayarishaji mshiriki wa wimbo "You Are the One for Me," ambao ulikuwa rekodi ya mwisho kufanywa na kundi la GQ. Mmoja wa wanachama waanzilishi wa GQ ni mjomba wake, Keith "Sabu" Crier.[11]

1992–2001: Get Up on It, Keith Sweat/LSG

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1992, Sweat alianzisha kundi la Silk, na kusaidia kutengeneza albamu yao ya kwanza, Lose Control, ambayo ilishika namba 7 kwenye chati za albamu za Billboard 200.[12] Wimbo wa kundi hilo "Freak Me" ulishika namba 1 kwenye chati za Billboard Hot 100 mnamo Mei 1, 1993.

Mwaka 1993, Sweat alianzisha kundi la kike la R&B la mjini Atlanta linaloitwa Kut Klose. Alitayarisha albamu yao ya kwanza Surrender, iliyotoa wimbo wao maarufu "I Like", ulioshika namba 8 kwenye chati za R&B/Hip-Hop.

Mwishoni mwa mwaka 1994, Sweat alionekana kwenye kundi la Black Men United (BMU) akiungana na Silk, Gerald Levert, Al B. Sure!, Brian McKnight, El DeBarge na wengine kwa ajili ya wimbo "U Will Know".

Sweat alitoa albamu yake ya nne Get Up on It msimu wa joto wa 1994, na albamu yake ya tano yenye jina lake mwenyewe mnamo 1996. Zote mbili ziliingia kumi bora za Billboard 200. Wimbo wa "Twisted" akimshirikisha Kut Klose ulishika namba 2 kwenye Billboard Hot 100 na "Nobody" ukashika namba 3, ambazo zikawa rekodi zake zilizofanya vizuri zaidi hadi leo. Alitayarisha pia kundi la R&B la Dru Hill mwaka 1996.

Mnamo 1997, alianzisha kundi la Ol' Skool na kusaidia kwenye albamu yao. Sweat pia aliunda kundi la mastaa la LSG akishirikiana na Gerald Levert na Johnny Gill, na kutoa albamu ya Levert.Sweat.Gill mwezi Novemba mwaka huo. Albamu hiyo ilijumuisha wimbo "My Body", uliokuwa kishindo kikubwa.

Albamu yake ya sita, Still in the Game, ilitoka mwaka 1998 ikishika namba 6 kwenye Billboard 200. Ilikuwa na nyimbo kama "Come and Get With Me" (akimshirikisha Snoop Dogg). Mafanikio yake kwenye chati yalianza kupungua mwaka 2000 alipotoa albamu ya Didn't See Me Coming.

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Kuanzia mwaka 1992 hadi 2002, Sweat alikuwa amemuoa nyota wa kipindi cha The Real Housewives of Atlanta, Lisa Wu Hartwell. Alizaa naye watoto wawili wa kiume, waliozaliwa mwaka 1995 na 1998.[13][14]

Pia ana mabinti watatu, mmoja akizaa na Tracy J. Pia ana mtoto wa kiume anayeitwa Joshua.[13]

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]
Albamu za studio
Albamu za ushirikiano
MwakaJinaUhusikaMaelezo
1991New Jack CityMwimbaji harusini
2000RhapsodyWillFilamu ya TV
2006Forbidden FruitsTerrenceVideo
2009Pastor BrownNasim
2018Love MagicalDelonte Skywalker
2021For the Love of MoneyChris
2023You're Not AloneJohnson

Televisheni

[hariri | hariri chanzo]
MwakaJinaUhusikaMaelezo
1988Showtime at the ApolloMwenyewe/MgeniSehemu: "Episode #2.10"
1994New York UndercoverMwenyeweSehemu: "Mate"
1997MartinDet. Carl JohnsonSehemu: "Stake-Out"
1997The Wayans Bros.MwenyeweMgeni: Misimu 3-4
2011The GameMwenyeweSehemu: "Death Becomes Her"
2017Hell's KitchenMwenyeweSehemu: "Raising the Bar"

Tuzo na teuzi

[hariri | hariri chanzo]
  • American Music Awards
    • 1991: Favorite R&B/Soul Male Artist (alipendekezwa)
    • 1997: Favorite Male R&B/Soul Artist (Mshindi)
    • 1997: Favorite R&B/Soul Album (Keith Sweat) (alipendekezwa)
    • 1998: Favorite Male R&B/Soul Artist (alipendekezwa)
    • 2013: Soul Train Lifetime Achievement Award
  1. ↑ Johnson, Connie (1988-03-20). "Keith Sweat: From Stock Market to Pop Market". Los Angeles Times (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-10-15.
  2. ↑ Eggert, Mike (1999). "Keith Sweat". Katika Phelps, Shirelle (mhr.). Contemporary Black Biography: Profiles from the International Black Community. Juz. la 19. Detroit: Gale. ku. 205–207. Iliwekwa mnamo Julai 8, 2025 – kutoka Internet Archive.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. ↑ Ruhlmann, William. "Keith Sweat Biography". allmusic. Iliwekwa mnamo Julai 8, 2025.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 1 2 Dougherty, Steve; Little, Benilde (Septemba 26, 1988). "Keith Sweat Takes Stock of His Talent and Puts Wall Street Behind Him". People Weekly. Juz. 30, na. 13. uk. 115.{{cite magazine}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. ↑ "Harlem-born R&B singer and radio host Keith Sweat releases new album". Welcome to Harlem (kwa Kiingereza). Desemba 4, 2011. Iliwekwa mnamo Oktoba 15, 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)[dead link]
  6. ↑ "Keith Sweat". WLA Talent Agency (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-10-15.
  7. ↑ "Keith Sweat shares thoughts on success". The Philadelphia Tribune (kwa Kiingereza). 2012-08-13. Iliwekwa mnamo 2024-10-15. [dead link]
  8. ↑ Dougherty, Steve (Januari 27, 1997), "For love and money", People Weekly, juz. 47, na. 3, uk. 69{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. ↑ "About". KeithSweat.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Februari 20, 2017. Iliwekwa mnamo Februari 27, 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. ↑ "Keith Sweat". iFLYER. Iliwekwa mnamo 2024-10-15.
  11. ↑ David Hinckley (Oktoba 1, 2013). "Keith 'Sabu' Crier, bass player for disco group GQ, dead at 58". Daily News.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. ↑ "Silk Chart History > Billboard 200". Billboard. Iliwekwa mnamo 22 Januari 2022.{{cite magazine}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  13. 1 2 "CBSi". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Juni 14, 2012. Iliwekwa mnamo Juni 26, 2016 – kutoka Find Articles.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. ↑ "Real Housewives of Atlanta: Ed and Lisa Wu Hartwell". Essence. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Desemba 22, 2014. Iliwekwa mnamo Machi 4, 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]