Nenda kwa yaliyomo

Hansi Flick

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hansi Flick
noborder
Hansi Flick mnamo 2022
Taarifa binafsi
Jina kamiliHans-Dieter Flick
Tarehe ya kuzaliwa24 Februari 1965 (1965-02-24) (umri 61)
Mahali pa kuzaliwaHeidelberg, Ujerumani
Kimo1.77 m (5 ft 9 1⁄2 in)
Taarifa za klabu
Klabu ya sasaBarcelona (Kocha Mkuu)
Kazi katika klabu
MiakaTimuMechi†(Goli)†
1982–1985SV Sandhausen
1985–1990Bayern Munich104(5)
1990–1993FC Köln44(1)
1994–2000FC Victoria Bammental
Timu ya Taifa ‡
1983Ujerumani U182(0)
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only and correct as of 8 Agosti 2026.

† Appearances (Goals).

‡ National team caps and goals correct as of 8 Agosti 2026

Hans-Dieter "Hansi" Flick (alizaliwa 24 Februari 1965) ni kocha wa mpira wa miguu na mchezaji wa zamani kutoka Ujerumani, ambaye sasa ni kocha mkuu wa klabu ya ligi ya La Liga, FC Barcelona. Anachukuliwa kuwa mmoja wa makocha bora zaidi duniani.[1][2]

Maisha ya awali na uchezaji

Katika enzi zake za uchezaji, Flick alikuwa kiungo wa kati aliyecheza mechi 104 na kufunga mabao matano akiwa na klabu ya Bayern Munich kati ya mwaka 1985 na 1990.[3] Akiwa na Bayern Munich, alitwaa ubingwa wa Bundesliga mara nne pamoja na taji la DFB-Pokal, na alicheza fainali ya European Cup mnamo mwaka 1987.[4]

Baadae alijiunga na FC Köln ambapo alicheza mechi 44 kabla ya kulazimika kustafu soka la kulipwa mwaka 1993 kutokana na majeraha. Alitamatisha soka la ushindani katika klabu ya Victoria Bammental kuanzia mwaka 1994 hadi 2000.[5]

Ingawa hakuwahi kuchezea Timu ya taifa ya wakubwa ya Ujerumani, Flick aliiwakilisha nchi yake katika timu ya vijana ya chini ya umri wa miaka 18 (U18) mara mbili mnamo Mei 1983 kwenye mashindano ya UEFA European U-18 Championship.[6]

Kazi ya ukocha

Hatua za awali na TSG Hoffenheim

Flick alianzia safari yake ya ukocha mwaka 1996 akiwa kocha-mchezaji wa Victoria Bammental. Mnamo mwaka 2000, alitangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya TSG 1899 Hoffenheim, ambapo aliipandisha daraja hadi Regionalliga Süd katika msimu wake wa kwanza, pamoja na kushinda taji la North Baden Cup mara nne mfululizo kuanzia mwaka 2002 hadi 2005.[7]

Timu ya Taifa ya Ujerumani

Mnamo 23 Agosti 2006, aliteuliwa kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Ujerumani chini ya kocha mkuu Joachim Löw. Katika kipindi hiki, alikuwa sehemu ya mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kutinga fainali ya UEFA Euro 2008, kushika nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia la FIFA 2010, na hatimaye kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia la FIFA 2014. Baada ya ubingwa huo, alihudumu kama mkurugenzi wa michezo wa Shirikisho la Soka la Ujerumani (DFB) hadi Januari 2017.[8]

Mnamo Mei 2021, alirejea kwenye timu ya taifa kama kocha mkuu akichukua nafasi ya Joachim Löw baada ya kukamilika kwa UEFA Euro 2020.[9] Aliiwezesha Ujerumani kufuzu kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA 2022, lakini kufuatia matokeo yasiyoridhisha ya kuondolewa katika hatua ya makundi pamoja na mfululizo wa matokeo mabaya kwenye mechi za kirafiki, aliondolewa kwenye nafasi hiyo mnamo Septemba 2023.[10]

FC Bayern Munich

Flick alirejea Bayern Munich kama kocha msaidizi mnamo Julai 2019 chini ya Niko Kovač. Baada ya Kovač kuondoka mnamo Novemba 2019, Flick alipewa mikoba ya kuwa kocha wa muda na baadaye alithibitishwa kuwa kocha mkuu kuingoza klabu hiyo.[11]

Katika msimu wa 2019–20, aliiongoza Bayern Munich kutwaa ubingwa wa Bundesliga, DFB-Pokal, na UEFA Champions League, akitimiza mafanikio ya kutwaa mataji matatu makubwa (treble).[12] Baadae alishinda pia UEFA Super Cup na FIFA Club World Cup, na kuungana na Pep Guardiola na Luis Enrique kama makocha pekee waliowahi kushinda mataji sita (sextuple) ndani ya mwaka mmoja.

FC Barcelona

Mnamo mwaka 2024, Flick aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya FC Barcelona inayoshiriki La Liga nchini Hispania.

Marejeo

  1. ↑ Karlsen, Tor-Kristian (2025-08-12). "Ranking the top 30 best men's club managers in Europe". ESPN.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-09-26.
  2. ↑ White, Mark; Mewis, Joe; Stronge, Isaac Stacey; Nee, Chris; Holt, Matthew (2025-06-25). "Ranked! The 50 best managers in the world right now". FourFourTwo (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-02-13.
  3. ↑ "Flick, Hans-Dieter". Kicker (kwa Kijerumani). Nuremberg: kicker. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Oktoba 2019. Iliwekwa mnamo 26 Mei 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. ↑ "Hansi Flick: 10 things on Bayern Munich's record-breaking, treble-winning coach". Bundesliga. Agosti 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Mei 2021. Iliwekwa mnamo 25 Mei 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. ↑ "Hansi Flick: Vom Assistenten zum Triple-Sieger und Bundestrainer" (kwa Kijerumani). Frankfurter Rundschau. 14 Machi 2022. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Desemba 2023. Iliwekwa mnamo 10 Septemba 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. ↑ "Flick: "I have a more relaxed approach now"". DFB. 23 Februari 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Juni 2024. Iliwekwa mnamo 10 Septemba 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. ↑ "Flick als Co-Trainer der DFB-Auswahl vorgestellt – Köpke verlängert bis 2008" [Flick introduced as assistant coach of the DFB national team – Köpke extends until 2008]. dfb.de (kwa Kijerumani). Frankfurt: DFB. 24 Agosti 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Novemba 2019. Iliwekwa mnamo 6 Novemba 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. ↑ "DFB stimmt Wunsch von Flick nach Vertragsauflösung zu" [DFB agrees to Flick's request for contract termination]. dfb.de (kwa Kijerumani). Frankfurt: DFB. 16 Januari 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 16 Januari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. ↑ "Hansi Flick wird neuer Bundestrainer" [Hansi Flick is the new national coach]. German Football Association (kwa Kijerumani). 25 Mei 2021. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Mei 2021. Iliwekwa mnamo 25 Mei 2021.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. ↑ "Three defeats in a row! Sorry Germany thrashed 4-1 by Japan to leave Hansi Flick's job hanging by a thread". Goal.com. 9 Septemba 2023. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Desemba 2023. Iliwekwa mnamo 10 Septemba 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. ↑ "FC Bayern and head coach Niko Kovac part company". fcbayern.com. Bayern Munich. 3 Novemba 2019. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Novemba 2019. Iliwekwa mnamo 3 Novemba 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. ↑ "Bayern beat PSG to win Champions League". BBC Sport. 23 Agosti 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo 24 Agosti 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)